ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 18, 2015

KINANA WILAYANI MBOGWE, GEITA, JANA JUNI 17, 2015

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Kata ya Masumbwe, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdylrahman Kinana uliofanyika katika kata ya Masumbwe, wilayani Mbogwe mkoani Geita, jana Juni 17, 2015.
Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdlrahman Kinana alipohutubia maelfu ya watu katika mkutano wa hadhara uliofanya katik kata ya Masumbwe, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya Kata ya Kashelo, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015.
Wananchi wa Kata ya Kshelo, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa zahanati yao, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapokea wanachama wapya wa CCM, waliohama kutoka Chadema, katika mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Lugunga, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na kijanaAugustine Gerald na kuahidi kumpeleka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), alipokagua ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Kijiji cha Lugunga, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 17, 2015
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivuka kwenye daraja duni, wakati akienda kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji cha Lyamchele, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita, jana, Juni 16, 2015. Tayari serikali imeanza mpango wa ujenzi wa daraja imara katika Kijiji hicho.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisafirishwa kwa pikipiki, baada ya kuvuka daraja duni kwenda kijiji cha Lyamchele kukagua ujenzi wa shule, utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, jana, Juni 16, 2015.
Wananchi wa Kijiji cha Lyamchele, wakiwasindikiza kwa ngoma na Kisukuma, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji hicho, Juni 16, 2015
Vijana wanaojishughulisha na kutafuta madini ktika udongo wa masalia, wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana

No comments: