MAALIM SEIF AMUWAKILISHA DK. SHEIN KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MUZIKI KWA NCHI ZA JAHAZI
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwamuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, katika ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa muziki kwa nchi za jahazi, inaofanyika chuo cha muziki Forodhani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Chuo cha Muziki Zanzibar bibi Fatma Kilua, akimkaribisha mgeni rasmi Maalim Seif katika ufunguzi za mkutano huo.
Muandaaji wa mkutano huo Profesa Raymond Vogals, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano huo wa kimataifa wa muziki, wakisikiliza hotuba
ya mgeni rasmi Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kwa niaba ya Dkt. Shein.
Mwanafunzi wa Diploma katika chuo cha muziki Zanzibar Gora Mohamed (kulia), akitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa muziki, baada ya kuufungua rasmi huko chuo cha muziki Forodhani Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa kimataifa wa muziki unaofanyika chuo cha muziki Forodhani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment