ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 11, 2015

Membe: Nikikatwa Nitampigia Kampeni Profesa Mwandosya


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kama CCM haitampitisha kuingia tano bora, atampigia kampeni kwa moyo wa dhati Profesa Mark Mwandosya iwapo ataingia fainali ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.
Membe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya waliojitokeza kumdhamini.

Alisema unapozungumzia viongozi waadilifu nchini, Profesa Mwandosya ni namba moja, kwani amekuwa kiongozi mwenye maadili ya uongozi na mwenye upendo wa dhati kwa wengine.

“Natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina langu lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya. Sina tatizo lolote hata wakisema mimi nimuachie Mwandosya nipo tayari, kwani ndiyo viongozi wanaotakiwa kama yeye kwa sasa kuongoza nchi yetu,” alisema.

Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mmoja wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakieleza kuwa wameamua kuingia kwenye mbio hizo kwa kuwa hawajaona mgombea mwenye sifa zaidi yao.

Wakati akitangaza nia ya kugombea urais mkoani Lindi, Membe alisema: 

“Nimetafakari sana kuhusu urais nimeona niombe. Nimejilinganisha na watu wengine wote wanaotia nia, na baada ya kumpitia mmoja baada ya mwingine, nimeona Lindi tuna nafasi ya kuchukua na kuwa na kiongozi wa juu Tanzania.”

Na baada ya kuzungumza kwa kirefu aliuhoji umati akisema, “nani kama Membe?” na kujibiwa “hakuna”.

Kuhusu mipango yake kwa Mkoa wa Mbeya, alisema anatarajia kuboresha huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa kuwa ni kitovu cha uchumi.

Awali katibu wa CCM wa mkoa, Alhaji Mwangi Kundya alisema jumla ya wanachama 877 walijitokeza kumdhamini Membe licha ya kwamba wanaotakiwa ni 30 tu.

7 comments:

Anonymous said...

Hii ni chance ya mwandosya honesty speaking .Wengine Kama January makamna ni entitlement mentality na arrogance .Mwandosya ameshawahi kushika nyadhifa za executive level ( katibu Mkuu wizara ya nishati na madini ) .Wengine Hapo ni WIZI tuuu.

Anonymous said...

Membe kaweka wazi, ili CCM wajihakikishie ushindi zidi ya UKAWA watatakiwa wamteue Mwandosya au Magufuli, wakishindwa sana yeye Membe. Kwa wagombea wengine initakuwa kazi sana kuwauza, wengine hawauziki ndio inaweza ikawa mwisho wa CCM. Kwa mfano wakimsimasha Lowassa, hakuna anayeweza kumtetea kwamba hakuhusika na wizi wa Richmond, kwa kuwa alikubali mwenyewe wakati wa kujiuzulu mwaka 2008, pia wengine wengi wana kashfa nyingi tu za kina ESSCROW. Kwa mfano wa January na Mwigulu, hawana uzoefu wowote, hawajawahi kuongoza hata Wizara. Vilevile Wizara ya fedha ina kashfa nyingi mpaka sasa, ESSCROW iliwagusa hata wizara ya fedha, pia ripoti ya CAG ya mwezi uliopita imeonyesha mapungufu mengi sana ndani ya wizara ya fedha. " Chama kwanza mtu/ rafiki baadae.

Anonymous said...

Mwandosya is sick.We cant afford to have another election.

Anonymous said...

Maadili pekeee hayatoshi kuiongoza nchi hii yenye changamoto kibao na iliyojaa wajanja,wezi, watu wasiopenda kuwajibika,wakwepa kodi etc..
Mwandosya he is too soft kukabiliana na hayo..
Magufuli ndio atakaeuweza mfupa huu..

Anonymous said...

Kila mtu ni mgonjwa hata wewe mwenyewe ni mgonjwa. Kila mtu anatembea na kifo kila siku. Ni MUNGU peke yake anayejua hatima maisha yetu.

Anonymous said...

Acheni siasa za maji machafu na muache kuishi Kwa kukaliri hiyo Richmond ndio iko pale ubungo mpk leo dowans this means ingekuwa haifai wasingeiruhusu kufanya kazi but kiburi mna kazi Richmond Richmond mbona baada ya kustaafu hamkuvunja mkataba tena mpk marais wa us Obama na bil clinton wenyewe wamesithibitisha kuwa mkataba haukuwa na tatizo but bado tu mnakaliri mnazani jinsi nchi ilivyo sasa ivi hao mnaowataka wataiweza zaidi ya kutupeleka gizani alafu mbakaza nyerere alimkataa Hahahaha kikwete mlisema ivyo ivyo huyu nae ivyo ivyo tusipende ushabiki mavi

Anonymous said...

Kwanza wewe hujui unachosema pole sana. Hao marais wa Marekani unaowasema hawakuwepo madarakani wakati huo, hiyo ni njaa inakusumbua umepewa vijisenti ndio unapiga ngebe. Sisi tunazumngumza ukweli tupu, hao unaowaona kujitokeza kumdhamini ni mamruki wachache wa CCM walionunuliwa ambao ni sehemu ndogo sana ya Watanzania watakaopiga kura.. Kumbuka watakaopiga kura Oktoba ni Watanzania wote, sio wana CCM pekee. Kumbukumbu zote za sakata zima la Richmond watu wanazo, na zitawekwa wazi na UKAWA wakati ukifika ili umma ujikumbushe yaliyojiri wakati huo 2008, vilevile wasioyajua waweze kuyajua. Sasa ikifika hapo UKAWA watajichukulia nchi kilaini. Yatawekwa wazi yote ya kina Rostam Aziz, Karamagi, Msabaha, Lowassa na vijisenti (Chenge). Kwa kufahamu hayo ndio maana mwenyekiti akaweka wazi "chama kwanza rafiki / mtu baadae.