Taasisi ya John Mashaka Foundation
pamoja na American Engineering Group (AEG) hatimaye imeweza kuwasaidia
wanakijiji 3,500 katika kijiji cha Manila wilayani Rorya kupata maji safi na
salama. Mradi huu umegharamu kiasi cha
Shilling Billion moja. Kabla ya huu mradi wananchi wa hiki kijiji walikuwa
wakitembea kilometa 24 kwenda ziwani na kurudi. Kazi ambayo ilikuwa ikifanywa
na watoto pamoja ba wanawake.
Huu ni mradi wa aina yake, kwani unatoa maji safi na salama. Na ina uwezo wa kusafisha kiasi cha lita 100,000 kwa siku ambayo inakuwa safi na salama. Kwa kiwango cha 99.9%. Mitambo hii imeagizwa moja kwa moja kutoka Marekani, ambaki ilibuniwa kwa namna yoyte ile ile. Inajitegemea na kujiendesha kwa kutumia nishati ya jua. Pampu ya maji ina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 20.
Tembelea tovuti ya John Mashaka Foundation kwa kubonyeza hapa
Mafundi wakishauriana jamba. Huu mtambo unaweza kupandisha maji lita 20,000 kwa saa. Hufanya kazi kwa kutumia solar. Na unachuja maji kwa 99.99% kuwa safi na salama

Mkuu wa mkoa wa Mara, Col. (Rtd) Aseri Msangi akiongea na wanakijiji kuhusu manufaa ya huu mradi wa maji kwenye maisha yao
Mafundi wakichota maji kwenye kisima cha zamani, ambayo yalikua ya msimu
Mafundi wakishauriana jamba. Huu mtambo unaweza kupandisha maji lita 20,000 kwa saa. Hufanya kazi kwa kutumia solar. Na unachuja maji kwa 99.99% kuwa safi na salama
Tembelea tovuti ya John Mashaka Foundation kwa kubonyeza hapa







2 comments:
Safi sana Mungu ambariki
Kitu simple kama kuvuta maji na pump hadi msaada wa Wazungu? Mxxhhh!
Post a Comment