ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 22, 2015

PASSPORT RENEWAL SEATTLE, WASHINGTON STATE

Jumuiya ya Tanzaseattle kwa kushirikiano na wenzetu wa Portland na Idaho tulipitisha wazo la kushirikiana kumleta Ofisa wa Uhamiaji kutoka Ubalozi wetu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania uliopo Washington DC.

Watanzania mbali mbali wa maeneo tajwa wamejitokeza kujiandikisha kwa ajili ya zoezi hili. Ada ya malipo kwa ajili ya kumleta ofisa wa ubalozi kila mshiriki ni US $45. Jumuiya inatoa shukrani za dhati kwa wale wote ambao wamesha wasilisha ada hiyo. Pia Jumuiya inawaomba wale wote ambao bado hawajawasilisha ada zao wafanye hivyo haraka ipasavyo kupitia akaunti ya Tanzaseattle KeyBank # 477991002247(Tafadhali weka risiti ya malipo). Au wanaweza kuwasilisha malipo ya pesa taslim(cash) siku ya kufanyika zoezi hili.. (Never too late).

RATIBA NA ADA YA MALIPO YA PASIPOTI( United Republic of Tanzania Passport).

Jumamosi TAREHE 27/6/2015 - Kuanzia saa Tatu asubuhi(9am) - Kumaliza saa Kumi na moja jioni(5pm).
Jumapili TAREHE 28/6/2015 - Kuanzia saa Tatu asubuhi(9am) - Kumaliza saa Kumi na moja jioni(5pm)

Ada ya malipo ya Pasipoti kwa kila Muombaji ni US $50
Ada ya malipo ya Posta kutumiwa Pasipoti ni US $20
Malipo haya kwa ofisa wa Ubalozi yatalipwa kwa MONEY ORDER siku ya Kujiandikisha.
Vitu vinavyohitajika kwa Muombaji.
Kopi Tano za Picha( Passport size 2 by 2 with Light Blue Background)
Kopi ya Pasipoti-Ukurasa wa kwanza(First Page) na Ukurasa wa Mwisho(Back Page)
Kopi ya Identification Card i.e Driver Licence
Kwa ambao watafanya maombi kwa ajili ya watoto wao wanaombwa kuja na Kopi ya Cheti cha Kuzaliwa cha Mtoto pamoja na Kopi ya Cheti cha kuzaliwa cha Baba au Mama wa Mtoto.

Anuani ya Pahala ni:
411 156th Ave Ne, 
Bellevue WA 98007.

Common Landmark to the address location is Crossroad Mall in Bellevue WA.
Kwa wale wageni wanaweza kuwasiliana na wafuatao pindi kutatokezea tatizo la kupotea njia.

1. Emil Muta: 206 291 8835
2.Haji R. Haji 206 302 9404
3.Jimmy Mkude 206 499 7054
4. Abdul Dola aka (Mayor of Seattle) 206 422 3050.

TUNAOMBWA TUZINGATIE MUDA ULIOPANGWA.

Jumuiya ya TanzaSeattle inapenda pia kuwatakia Kheri na Baraka waislamu wote kwa kutekeleza mfungo wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani. Kheri na Baraka kwa Watanzania wote.

Ahsanteni Sana.

Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Tanzaseattle.

Wenu,

Katibu Tanzaseattle- Haji Rajab Haji.

No comments: