Advertisements

Monday, June 1, 2015

TASWIRA YA MISA YA KUMUOMBEA MZEE LUANGISA ILIYOFANYIKA NEW YORK

Maura Mwingira, Charge d' affaires a.i wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akitoa pole kwa watoto wa Mzee Luangisa kwa niaba ya balozi alipata nafasi ya kuongea machache mbele ya Watanzania waliojitokeza kwenye misa hiyo ya kumuombea marehemu mzee Luangisa pamoja na kuaga mwili wake tayari kwa safari ya kwenda nyumbani Bukoba Tanzania kwa mazishi yatakayo fanyika jumanne ya tarehe 2.
Mtoto wa marehem Kwame akitoa wasifu wa mzee Luangisa wasifu huo uliwatoa machozi watu kutokana jinsi mzee Luagisa alivyokuwa mtu mwenye moyo wa kutoa kwakile alichonacho bila kuchagua wala kuhoji.

Mayor wa Mt Vernon, New York bwana Ernest Davis akiongea machache mbele ya Watanzania kwenye misa hiyo ya kumuaga mzee Luangisa.
Mchungaji akiongoza misa mbele ya Watanzania wa New York na miji ya karibu na New York.
Watoto wa marehem wakiwa na sura za udhuni ya kuondokiwa na baba yao mpendwa ambae alikuwa nguzo ya familia hii pendwa.
Watu wakiaaga mwili wa mzee Luangisa pamoja na misa iliyofanyika jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa 5. Kwa picha zaidi nenda soma zaidi.

Kwa picha zaidi tembelea  http://tembaphoto.com/

No comments: