ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 9, 2015

UNANINI CHA KUSEMA JUU YA MANENO HAYA YA PROF ANNA TIBAIJUKA KWA WAPIGA KULA WAKE BAADA KUZOMEWA MBELE YA KINANA HUKO BUKOBA.

JE mnachuliaje uamuzi alichokua Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) na aliewahi kuwa waziri wa Ardhi nyumba na makazi, 
Profesa Anna Tibaijuka jana baada ya kuzomewa mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambapo alisema haya
“Kama hamnitaki siyo lazima niwe mbunge wenu, mnaruhusiwa kubadili. Huyo aliyewapa viroba asubuhi hii ili mje mnitie aibu mbele ya katibu mkuu wa chama nawaambia hiyo dhambi itawatafuna,” alisema. “Mimi sitafuti kazi na wala sina njaa... na kama hela ya kula ninayo. Mimi sigangi njaa na kama mnataka kuwa na kiongozi mganga njaa muwekeni muone atawasaidia vipi,”:

Chanzo:mwananchi 

Je una maoni gan juu ya kauli za mbunge huyu??





7 comments:

Anonymous said...


My opion: Mama huyu ndio kiongozi bora- she does not give " what..": Kinongizi masikini hawezi kuendesha nchi masikini.

Anonymous said...

Mama bado ana kiburi cha 1.6 billion. Anatakiwa arudishe ndiyo atakuwa na adabu.

Anonymous said...

KAULI YA MHE, TIBAIJUKA NI SAHIHI NA NDIYO UKWELI WENYEWE HAKUNA HAJA YA KUBEMBELEZA WATU WASIOJITAMBUA WALIKUWA WAPI MIAKA ILIYOPITA NAKUBALIANA NA DC KUWA AMBAYE HATAKI KUSIKILIZA AONDOKE WABAKI WENGI WAO WALIO TAYARI, TUACHE SIASA ZA MAJI TAKA ZA KUTUMA WATU WA KUZOMEA WATU

Anonymous said...

MTENDA AKITENDEWA HUJIONA KAONEWA, WAO WAMETUKANA WALIVYOWEZA MBELE YA KINANA NAYE KAMA BINADAMU AKAJIBU, SASA YEYE SIO MUNGU WALA MALAIKA, NA NIVIZURI WASUBIRI BOX LA KURA WAAMUE NA SIO KUTUKANA, HIVI NANI ALIYEMSAFI, YESU ALIWAULIZA WALE WALIOTAKA KUMPIGA YULE MWANAMKE KWA KUZINI WOTE ALIYE WA KWANZA ANAYEJIONA HANA DHAMBI NA SIO AMBAYE AMEWAHI KUPATA HELA KWA RUSHWA NA AWE WA KWANZA KUMPIGA HUYU MAMA,WANADHAMBI ZAO AMBAZO MIMI NA WEWE HATUZIJUI. TUACHE KUHUKUMU MWENYE KAZI HIYO YUPO NA AMETULIA.

Anonymous said...

Kazi kwelikweli, mamahuyu kafilisika kimawazo,mtizamo na hata malengo. Hajui alikotoka, aliko na anakoenda. Mfa maji haachi kutapatapa! Viongozikama hawa wenye kiburi kwa rushwa ndiyo wanaoiliafuna taifa. Jumuiya ya kimatifa ilimheshimu kwa kuwa hawakujua kuw ani mla rushwa na asiye na asiyejiheshimu. Zawadi nzuri ya kumpa ni kumuadhibu kwa kumnyimakura. Najua atatumia hela za Escrow alizopewa lakini wananchi wa Muleba mkataeni kwa kuwa 10,000 unayopewa ya kuganga njaa leo itakugarimu miaka 5 kwani hatakupa lolote zaidi ya kumuona kwenye tv(kama unayo) akiwa bungeni au mijini kuendelea kusaka wenye hela wengine ( Rewagasira).

Anonymous said...

Jeuri ya escrow! Vijisenti hivyo!

Anonymous said...

Mimi siyo mwanasiasa, lakini Mama hapo kakosea vibaya. Huwezi kuwatukana, kuwacheka , au kuwadharau wananchi irrespective of political tendencies. Tupo wasomi wengi Tanzania, na Matajiri wengi wanaibuka, lakini siyo busara kwa sisi wenye nafasi nzuri kihali na mali kuwaweka chini wale wasiobahatika, maana kufanya hivyo inatuaibisha Wasomi na Matajiri wote. Naona mama Tijaibuka AMESOMA SANA lakini HAJAELIMIKA!