Advertisements

Tuesday, June 30, 2015

USAFIRI UNAOTUMIKA KUSAFIRISHA ABIRIA MKOANI GEITA ENEO LA BUSERESERE NI HATARISHI

 
Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.
 Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo
Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya buseresere na katoro wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia Tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.
 
Gari Aina ya Pro Box Ikiwa tayari kusafirisha abiria
 Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria.

2 comments:

Anonymous said...

masikini Tanzania bado ni nchi ya ujamaa na kujitegemea

Anonymous said...

Halafu mheshimiwa sana katibu Mkuu tena wa Chama Tawala Kinana na timu ya msema hovyo Nape wanaenda kungangana CCM imefanya mengi yapi hayo wananchi wanataabika kwa kiasi hiki. Viongozi wanapotembbelea mahali hawaambiwi ukweli wa matatizo ya wananchi.