Mtendaji Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha (kushoto) akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan baada ya kutiliana saini ya mkataba wa kujenga nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na umma mradi unaotarajiwa kujengwa Chalinze
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) kwa kushirikiana na Taasisi ya SUMA JKT imesainiana mkataba wa makubaliano wa ujenzi wa nyumba za kisasa za kuuza kwa askari na maofisa wa jeshi na Umma, tukio lililofanyika Juni 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Taasisi ya UTT PID iliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Dr. Gration Kamugisha na Taasisi ya SUMA JKT iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu Lt-Colonel, Felix Samillan huku mradi huo ukitegemea kuanza katika kipindi cha mwaka mpya wa fedha wa serikali Julai mwaka huu.
Aidha, nyumba zinazotarajiwa kujengwa zitakuwa ni za vyumba viwili na vitatu katika miundo mbalimbali na za kuvutia ambazo zitakuwa za mfumo wa kisasa kwa kuishi kifamilia pia.
Katika mkataba huo utatanguliwa na ujenzi wa nyumba za mfano katika eneo la Chalinze na mara baada ya ujenzi huo kukamilika, Nyumba za mradi zitajengwa kwa walengwa wote watakaokuwa wameomba na kukidhi vigezo muhimu vya kupata nyumba hizo.
UTT-PID inafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Pia wanaendesha miradi ya viwanja maeneo mbalimbali nchini ikwemo Bagamoyo, Chalinze Mkoa wa Pwani, Lindi, Kagera, Korogoro na mikoa mingine mingi.
No comments:
Post a Comment