Tarehe 29
Juni 2015, Mamlaka ya Bandari Tanzania imefungua rasmi Ofisi nchini Zambia.
Ofisi hizo zimefunguliwa katika Jiji la Lusaka.
Dhumuni
kubwa la Mamlaka ya Bandari kufungua ofisi hii Lusaka ni baada ya kuwepo
malalamiko kwa upande wa Zambia ambaye ni mteja wake mkubwa ya kuwepo
ukiritimba wa utoaji wa mizigo yao. Hivyo Mamlaka ikaona ni vema kuja kufungua
ofisi hapa Lusaka.
Sherehe za
ufunguzi wa ofisi hii ulihudhuriwa na Mhe Dkt. Charles Tizeba Naibu Waziri wa
Uchukuzi na viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. Ofisi za
Mamlaka ya Bandari zipo katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Lusaka Zambia.
Ofisi
hii imefunguliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Mhe Yamfwa Dingle Mukanga.
BALOZI
WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE. BALOZI GRACE J. MUJUMA AKIWA NA MHE. NAIBU
WAZIRI CHARLES TIZEBA UBALOZINI. MHE. TIZEBA ALIKWENDA KUMSALIMIA MHE. BALOZI
OFISINI KWAKE.
MHE
BALOZI NA MHE NAIBU WAZIRI WAKIKAGUA OFISI YA TPA NCHINI ZAMBIA KABLA YA
UFUNGUZI
WAFANYAKAZI
WA TPA WAKIANGALIA MAANDALIZI YANAVYOENDELEA
MHE
GRACE J. MUJUMA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA AKITOA HOTUBA WAKATI WA
SHEREHE ZA UFUNGUZI
VIONGOZI
WAANDAMIZI WAKIMSILIKIZA MHE. BALOZI HAYUPO PICHANI AKITOA HOTUBA
KAIMU
MKURUGENZI MKUU WA TPA BW A. MASSAWE
AKITOA HOTUBA WAKATI WA UFUNGUZI
No comments:
Post a Comment