Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.
Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.
Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."
Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.
Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.
Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.
Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.
Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.
Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.
Tulikotoka na mwanamke huyu:-
Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)
Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.
Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.
Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaƱo yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.
Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.
Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.
Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.
Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.
Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.
Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.
By Nevile pablo-JF

11 comments:
MKuu,huyu demu ni mchagga? Nauliza hivyo maana hizi tabia zinaonyesha ni za kichagga chagga.
Tukiondoa hilo swala la kubakwa, hivi ana(li)vyofanya huyu mama sio sawa na wanaume wengi wanavyofanya kwa wake zao?
For your information mimi ni me sio ke.
Nimesoma maelezo haya kwa masikitiko sana. Wanawake wengine hujali sana mali kuliko mahusiano katika ndoa. Na inaonyesha huyo mama anakiburi. Huwezi ukamfanya mumeo kama si mumeo. Baada ya kusema hayo, napendekeza kwamba utafute muda ukamsikilize, na pengine kutokana na tukio la kubakwa, atakuwa amejifunza jambo. Kumbuka una watoto naye, watoto wataumia zaidi kuliko wewe kumkosa mama yao.
Jay tena ukome wachagga uwaache, you don't even know who the person is, it might be your sister from another mother. mama au baba yako ndio mchagga, uliyajulia wapi. Nyie ndo wale waleeee. Yes, mimi ni mchaga married to another tribe. Beautiful married full maendeleo, sijawahi na wala sitowahi kumdharau au kufanya alichofanya huyo dada. Ni tabia mbaya ya mtu. Narudia tena ukome.
Nakubaliana na wewe Kaka kwa maamuzi utakayoyofanya. Huwezi ukakaa ktk ndoa yenye migogoro na mapishano kisa watoto. Mwanamke alikuona hufai na wala huna umuhimu ktk maisha yake na kutokana na maelezo yako ni kuwa Mama yake alikuwa ndiyo mshauri wake mkubwa. Kama huyo Mke wako na Mama Mkwe wako wangeona umeoa na una watoto wasingediriki kukufanyia hayo, ila Mwenyezi Mungu amewaadhibu wote kwa njia tofauti. Wazazi wengi hasa wa kike huchangia kuvunja ndoa za wanao, hivyo ni jukumu la akina dada kuwa makini na hili kwani waathirika ni watoto wao zaidi na ikumbukwe kuwa uwezekano wa mwanamke kuoelewa tena akiwa na watoto ni mdogo ikilinganishwa na mwanaume. Hizi tabia si kwa wanawake wa kichaga tu ila ni kwa makabila yote. Kuna msemo usemao" Mwanamke Mwalimu wake ni Kipofu " Je unajua nini maana halisi ya memo huo..? Kama hujui Nijuze, Nitakujuza..
kila siku tunarudi pale pale kwa nini victim wa kubakwa analaumiwa? hapo mmeshaona makosa ni yake na yale mashetani ya segerea hamyaongelei, kwa nini hamkemei hayo mashetani mabakaji mmeanzisha hotuba za kumshutumu huyu mama? wakati anatafuta pesa na kuleta maendeleo nyumbani mnasifia mwanamke anajua kuhangaika leo kakutana na ajali ya kubakwa mnageuka acheni zenu hizo kemeeni yale mabakaji
wewe baba unachekesha kabisa kwa hiyo ulimpenda mama kwenye raha tu? unakumbuka kiapo ulichoapa mpaka kifo kitutenganishe kwa shida na raha kwa ugonjwa sasa mwenzako yamemfika unasepea wapi? ingekua mimi wewe ningehakikisha hao wabakaji na familia zao wote wanabakwa ningenunua wahuni wangejuta na kitendo walichofanya, kumuacha mke wako sio suluhisho unajitia ujinga tu hapo ulipo, kwanza ungeweka mambo kati yenu peke yenu mwanaume gani kitu kidogo unaitisha familia nzima mpaka mama yake, wewe mwenyewe ulishindwa nini kwenda peke yako?
Mnaolaumu mama kuficha document za mali zao acheni mara moja, ni kesi ngapi tunazisikia sisi wanawake tunadhulumika? nani kati yenu hajawahi kusikia? na huyu mama anafichiana siri na mama yake kuna ubaya gani? tena na baba unajua document anaziweka kwa mama mkwe, usipomuamini mama yako mzazi utamwamini nani duniani? mume mwenyewe yamekukuta ona unavyotimua zako, halafu ona nani yuko nawe mama mzazi, sioni ubaya wowote wa mke kuficha mali alizoachiwa na baba yake, mifano ni mingi sana imeshatokea wanawake wanakosa haki zao kila siku tunasikia nani tena aliye mjinga afanye yale yale yanayowakuta wenzake? ni mara ngapi mke na mume wanapendana wanajenga nyumba wananunua magari ugomvi ukizuka mke ndio anafukuzwa na kukosa kila kitu nani hajasikia hilo? alichofanya mke ni sahihi kabisa na alishakujua akikutwa na shida utamkimbia ona mfano hai umesema unampa talaka
Mnaolaumu mama kuficha document za mali zao acheni mara moja, ni kesi ngapi tunazisikia sisi wanawake tunadhulumika? nani kati yenu hajawahi kusikia? na huyu mama anafichiana siri na mama yake kuna ubaya gani? tena na baba unajua document anaziweka kwa mama mkwe, usipomuamini mama yako mzazi utamwamini nani duniani? mume mwenyewe yamekukuta ona unavyotimua zako, halafu ona nani yuko nawe mama mzazi, sioni ubaya wowote wa mke kuficha mali alizoachiwa na baba yake, mifano ni mingi sana imeshatokea wanawake wanakosa haki zao kila siku tunasikia nani tena aliye mjinga afanye yale yale yanayowakuta wenzake? ni mara ngapi mke na mume wanapendana wanajenga nyumba wananunua magari ugomvi ukizuka mke ndio anafukuzwa na kukosa kila kitu nani hajasikia hilo? alichofanya mke ni sahihi kabisa na alishakujua akikutwa na shida utamkimbia ona mfano hai umesema unampa talaka
Hasira zako zipeleke kwa wabakaji mama hajafanya lolote baya hata wewe linaweza kukufika wabaya wako ni wale wabakaji
Sikiliza sister wa June 21, 2015 at 1:46 AM, mimi ninaongea through experience. Hapa Bongo vijana wengi wanaogopa majinamizi ya talaka (wanawake wa kichagga) bcs hizi ndizo tabia zao, they are not marrying you for love but mali and hoping you die so they can inherit it and share with their family. Ahsante lakini kwa kujifanya unajali kwani I know una sababu zako. Kumbuka, asili haipotei, si ni mchagga wewe?
Post a Comment