Marehemu alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha
Kidia, Old Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.
Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kidia mwaka 1951 – 1954 na
baadae Shule ya Msingi Kidia Juu (Kidia Upper Primary School) mwaka1955 –
1958. Alihitimu Elimu ya Sekondari
Kidato cha Nne mwaka 1974 katika Shule ya Sekondari Mawenzi akiwa mtahiniwa wa
kujitegemea (Private Candate). Aidha, alisoma Cheti cha Sheria Chuo Kikuu cha
D’Salaam mwaka 1975 – 1976 na baadaye Shahada ya Kwanza ya Sheria Chuo Kikuu
cha D’Salaam mwaka 1977 – 1980.
Marehemu ajiunga na Jeshi
la Magereza mwaka 1964
baada ya kuhitimu Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Chuo Ukonga, D’Salaam
yaliyofanyika kuanzia Januari - Julai, 1964.
Ndani ya utumishi, alipata fursa ya kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi Daraja
la Pili (Advance Course) Chuo Ukonga, D’Salaam kuanzia Aprili – Julai, 1967 na
Mafunzo ya Uongozi wa Juu (Gazetted Course) kuanzia Februari – Mei, 1974.
Kutokana na utendaji wake wa kazi, marehemu
aliwahi kutunukiwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:-
·
Afisa Magereza Daraja la Tatu mwaka 1964
·
Afisa Magereza Daraja la Pili mwaka 1965
·
Afisa Magereza Mkuu Daraja la Nne mwaka
1967
·
Afisa Magereza Mkuu Daraja la Tatu
mwaka 1971
·
Mrakibu Msaidizi wa Magereza mwaka
1975
·
Mrakibu wa Magereza mwaka 1976
·
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza mwaka
1978
·
Kamishna Msaidizi wa Magereza mwaka
1982
·
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza mwaka 1984
·
Kamishna wa Magereza mwaka 1992
·
Kamishna Mkuu wa Magereza mwaka 1996 –
2002
Aliwahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali
vikiwemo Gereza Butimba - Mwanza, Isanga
- Dodoma, Wami Vijana - Morogoro, Chuo cha Usalama Moshi, Gereza Songwe - Mbeya, Chuo Ukonga - D’Salaam
na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, D’Salaam.
Aidha, marehemu aliwahi kushika nyadhifa
mbalimbali ndani ya Jeshi la Magereza kama ifuatavyo:-
·
Mkufunzi Mkuu Chuo Ukonga mwaka 1975
·
Mkuu wa Chuo Msaidizi, Chuo Ukonga
mwaka 1981
·
Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na
Urekebishaji, Makao Makuu mwaka 1983
·
Mkurugenzi wa Sheria na Urekebishaji,
Makao Makuu mwaka 1984
·
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Makao Makuu mwaka 1992
·
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza
mwaka 1996 – 2002 alipostaafu kazi.
Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa
alioutoa wakati wa utumishi wake. Baadhi
ya mambo aliyoyafanya ni kama ifuatavyo:-
·
Alianzisha na kuimarisha mahusiano
baina ya Jeshi la Magereza na Magereza ya nchi nyingine Afrika na duniani.
·
Alikuwa mmojawapo wa Makamishna wa Tume
ya Marekebisho ya Sheria Nchini (Law Reform Commission)
·
Alikuwa mshauri kwenye Maboresho ya
Jeshi la Magereza pamoja na Sera ya Taifa ya Magereza.
·
Kama hatua ya kupunguza msongamano wa
wafungwa magerezani aliweza kushauri na kusimamia
kutungwa kwa Sheria zifuatazo:-
-
Sheria ya Bodi ya Parole
-
Sheria ya Huduma kwa Jamii (Community
Service)
Nishani alizotunukiwa akiwa kazini ni:-
·
Nishani ya
mstari wa nyuma
·
Nishani ya
Utumishi mrefu
·
Nishani ya
Utumishi uliotukuka
Hata baada ya kustaafu kazi, marehemu aliendelea
kutoa mchango wake kwa kushauri mambo kadhaa pamoja na kushiriki kwenye matukio
mbalimbali ya Jeshi na Taifa. Kutokana
na mchango wake huo alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano
Daraja la Nne na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili,
2015.
Kwa niaba ya Kamishna
Jenerali wa Magereza na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza, tunatoa salamu
nyingi za rambirambi kwa Mke, Watoto na Ndugu wa Marehemu kwa msiba huo mkubwa
uliotufika.
MUNGU
AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA
No comments:
Post a Comment