Saturday, June 27, 2015

WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Iringa uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi. Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya Iringa.


..................................................................


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . 


Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika mikoa aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima, wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. 


Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.

No comments: