
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi na Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiweka jiwe la msingi katika nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi ambazo ujenzi wake utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimia
viongozi wa NHC mara baada ya kuwasili eneo la Napupa Masasi kuzindua
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC. Anayemuongoza Mh. Waziri ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi.

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na
hadhira iliyofurika katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama
nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.Alizitaka taasisi zinazotoa
huduma ya umeme na maji kutekeleza majukumu yao ili kupunguza gharama za
uuzaji wa nyumba zinazojengwa na waendelezaji wote wa makazi.

Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Masasi.
No comments:
Post a Comment