

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akizungumza na Bwana Karol Zarajczyk, ambaye ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland.
Na. Issa Sabuni, WKCU
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira amepongeza hatua iliyofikiwa katika ya Serikali ya Tanzania chini ya Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) na Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland akisifu kuwa hatua hiyo ni ya muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaongeza tija a uzalishaji katika kilimo lakini pia inapunguza matumizi ya jembe la mkono.
Waziri Wasira alipongeza hatua hiyo, mara baada ya kukutana na Bwana Karol Zarajczyk, ambaye ni Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland.
Waziri Wasira alisema hii ni hatua njema kwani, mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea Kampuni ya Ursus mapema mwaka huu, wawekezaji hao walikubali wazo la kushirikiana Kampuni ya SUMA JKT kwa ajili ya kuunganisha matrekta hapa nchi badala ya kuyaleta yakiwa yameshaunganishwa ambapo gharama yake ni kubwa zaidi, ambapo wakulima wengi watashindwa kumudu gharama ya kuyanunua.
No comments:
Post a Comment