Advertisements

Sunday, July 26, 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA WATANZANIA MAREKANI

Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa hotuba ya kuwaaga Watanzania wa Marekani waliokuja kutoka kila pembe ya Marekani siku ya Jumamosi Julai 25, 2015 nyumbani kwake Bethesda, Maryland. Boya Play usikilize alichoongea alipokua akiwaaga Watanzania wa Marekani.  Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
Mkuu wa Utawala mama Lily Munanka akisoma hotuba kwa niaba ua watumishi wa Ubalozi mahususi kwa ajili ya kumuaga Balozi Liberata Mulamula kwa kueleza masikitiko yake lakini wakimtakia utendaji wa kazi mwema huko aendako.
Kushoto ni Swahiba Mndeme na Mama Lily Munanka wakimkabidhi Balozi Liberata Mulamula zawadi kwa niaba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mama Lily Munanka Mkuu wa Utawala akimkabidhi zawadi Balozi Liberata Mulamula kwa ajili ya Mumewe Eng. George Mulamula ambaye kwa sasa yupo Nairobi, Kenya kuhudhuria mkutano wa Rais Obama.
Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akitoa hotuba yake kwa niaba ya watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York ambao watumishi wa Ubalozi huo wengi wao walikuwepo Bethesda kumuaga Balozi Liberata Mulamula.
Makamu wa Rais DMV Bi. Harriet Shangarai akitoa hotuba yake kwa niaba ya Jumuiya ya DMV.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Harriet Shangarai akimkabidhi Balozi Liberata Mulamula zawadi kwa niaba ya Uongozi wa DMV.
Abdul Majid akitoa salamu za California.
Akida akiwakilisha Jumuiya ya New York.
Viongozi wa DICOTA nao wakisema yao ya moyoni kutoka kushoto ni Dr. Kurwa, Dr. Mbilinyi na Ndaga Mwakabuta.
Viongozi wa DICOTA wakimzawadia Balozi Liberata Mulamula zawadi yao.
Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania North Carolina akiongea kwa niaba ya Watanzania wa North Carolina.
Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi ya Watanzania wa North Carolina.
Meza kuu.





3 comments:

Unknown said...

Your Honorable Mulamula, We Will All Miss You Greatly, Nimekumisi Kweli, Mungu Atubariki na Akubarikiwe Daima Milele, Tunakupenda Sana Milele.....

Anonymous said...

Hao ni wa-tz au wengine ni raia wa USA?..nusu au zaid ya waliohudhuria hiyo hafla sio wa-tz kwa maana walishaukana uraia wa tz na kuwa wamarekani...hii ni hatari kiusalama kwa ubalozi kuruhusu watu wasio wa-tz kuhudhuria kwenye official function ya nchi ya TZ.

Ubalozi unatakiwa kuwa makini sana na kuendesha mambo yake kwa protokali kama zilivyo nchi nyingine...haiwezekani leo mfano rais wa marekani akaenda tz na kutaka kuongea na raia wa marekani walio tz halafu ubalozi wa usa kule tz ukawaruhusu na raia wa-tz kuhudhuria. Mh. Magufuli akiingia atafagia huu uzembe!

mdau
Sweden

Anonymous said...

Tulipewa one day notice kwenye blogu hii, kwamba Watanzania wote hapa Marekani tunaalikwa pale Bethesda, kwenda kumuaga Mheshimiwa Balozi. It is puzzling to find people from Minnesota, Washington State, North Carolina, New York City, etc..kwenye attendace in such a short notice! What is going on? Apparently, some of us feel that, the processs of extending invitations is corrupt and somewhat selective, au pure ubaguzi? Vitu kama hivi ni pattern kule Bongo na siyo busara ku-import this outdated mentality huku ughaibuni. Ubalozi have to level the playing field, kwani wanatuwakilisha Watanzania wote na siyo the favored few. We hope and pray that, the coming President (Dr. Magufuli, definitely) will institute sweeping changes to the whole Foreign Affairs Ministry (from Top to Bottom), and impose new guidelines to those who serve and represent Tanzania and her people, overseas.