Advertisements

Wednesday, July 22, 2015

BREAKING NEWS: BASI LA SIMIYU LILILOKUWA LINATOKEA MWANZA KWENDA DAR LAPATA AJALI MKOANI DODOMA

Taarifa za mwanzo kutoka mkoani Dodoma zinasema kuwa Basi la Simiyu Expresslimepata ajali eneo la Chalinze - Mbande mkoani Dodoma na zaidi ya Abiria takribani 20 wamefariki dunia usiku huu, huku zaidi ya abiria zaidi ya 40 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma, hadi hivi sasa bado kuna miili haijatolewa kwenye mabaki ya basi hilo kutokana na kuharibika vibaya na kubaki mithili ya nyama.Na majruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.

ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAARIFA ZAIDI

No comments: