
Dodoma. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye pia alikuwa mwanamkakati katika kambi ya Edward Lowassa katika mbio za urais, amesema kambi yake inamuunga mkono mgombea urais aliyeteuliwa na chama kwa sababu anauzika.
Dk Nchimbi akizungumza na gazeti hili jana alisema Dk John Magufuli ni mgombea anayeuzika tofauti na wengine na kwamba kambi yao inamuunga mkono katika kukiwezesha chama kuendelea kushika dola.
Alisema linapofika suala la maslahi ya chama wote wanakuwa kitu kimoja na kwamba uwezo na utendaji wa Dk Magufuli ni wa hali ya juu, kiasi kwamba ni rahisi kumnadi kwa wananchi
.
Dk Nchimbi ambaye baada ya Kamati Kuu kutangaza majina matano ya wanaowania kuteuliwa, yeye na wajumbe wenzake wawili wa Kamati Kuu, Sophia Simba na Adam Kimbisa walitoka hadharani wakisema wanajitenga na maamuzi ya kamati hiyo kwa kuwa imekiuka katiba ya CCM.
Alisema baada ya vikao vya CCM kumpitisha Dk Magufuli, kambi yao imeamua kumuunga mkono kwakuwa ni mtendaji mzuri wa kazi anazopewa na mifano ipo mingi katika wizara alizoziongoza.
Dk Nchimbi alitoa mifano ya utendaji wa Dk Magufuli kwa kuwa ameweza kujenga barabara, kukamata meli za kigeni zinazovua kwa njia haramu katika bahari ya Tanzania na kupambana na ujenzi usiofuata sheria hasa kwenye maeneo ya barabara.
Mwananchi
3 comments:
Mnafiki mkubwa mchimbi wewe si timu Lowasa na ulikula hela yake uka ropoka wewe na hawara yako sofia simba kuwa lowasa ndio chaguo la wengi. Piga kimya acha unafiki,,, Dj luke usibanie comment yangu kama kawaida yako.
Wewe anon. hapo juu unaumwa? In politics, reconciliation is the name of the game for the country's good. Many of the 2104 voters including hawara zako may have been Membe or Lowasa supporters, BUT they casted their votes for Magufuli. Kama una bifu na Dr. Nchimbi, usimtumie Dj.Luke to express your frustrations. The country is moving on without Lowasa, too bad, if he was your potential messiah!
mnafiki njemba hii.lakini wakitaka wasitake mbona toka zamani jina la el lishakatwa.
movie inaendelea hii nasubiri kwa hamu.unadhani el atawaacha hivi hivi.ng'oo;labda wamkolimbe.
patachimbika labda wamtulize.kama alivyotuliza hii njemba
Anguko la dola Dharimu ni hizi dalili zake.
Post a Comment