ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 2, 2015

LEMUTUZ Aelezea Sababu ya Kutosomeshwa na Baba yake Ambae Alishawahi Kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Malecela


William Malecela, maarufu kama Lemutuz Nation au "King of All Bongo Social Networks" kama anavyofahamika katika mitandao mbalimbali ya kijamii ameeleza sababu za yeye kutosomeshwa na baba yake mzazi.
Le Mutuz Nation ambaye ametumia muda mwingi kusoma na kuishi nchini Marekani na Belgium, ameweka bayana katika kipindi cha Mlimanidotcom cha Mlimani TV kuwa alijisomesha kwa kupitia fedha ambazo zilitokana na kazi mbalimbali ambazo alikuwa akifanya kama vile udereva wa mabasi makubwa huko jijini New York pamoja na kukaanga kuku.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kujisomesha kupitia kuendesha malori na kukaanga kuku, Le Mutuz alisema “Liko sawasawa, unajua ni la ajabu Tanzania lakini si la ajabu nchi nyingine kwasababu mimi wakati nakua, tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa kwa hiyo mambo mengi yalikuwa yamebana na mimi nilikuwa nataka ubaharia”

Alieleza kuwa sababu kuu ni kuwa yeye alitaka ubaharia lakini baba yake hakutaka yeye asome masomo hayo katika ngazi ya chuo kikuu, Lakini pia ameeleza kuwa baba yake ambaye ni Waziri mkuu wa zamani wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hakumsomesha kwasababu kipindi yeye anakua ilikuwa ni kipindi cha ujamaa na mambo mengi yalikuwa yamebana hivyo baba yake asingeweza kumlipia kusoma nje ya nchi.

Pamoja na kueleza hayo, Lemutuz alizungumzia sababu za yeye kuliburuza gazeti la Kiu mahakamani na pia kwanini anapenda kupiga picha na wanawake na kuweka Instagram

2 comments:

Anonymous said...

sasa hizo sababu mbona hajatuelezea za yeye kuliburuza gazeti hilo na kupenda kupiga picha na wanawake.
jamaa naona amedata sasa;ebwana eeeh unawatoto wewe na sasa wanakuwa kuwa acha utoto bwana eeeh.unawatia aibu wanao kwa ushamba na ulibukeni wako wakutaka misifa katika mitandaoni.hukuwi wewe atii.unakuwa kama kuku boyaa kila siku aaah wacha hizo bwana eeeh.

mpeni ubunge jamaa atatulizana naona sasa anajipa promo mwenyewe.

sikusemi kwa ubaya au chuki jua nakupenda ndo maana nakuambiya haya William melecela le mutuz la nation le world le monde.le mbunge kampeni

Anonymous said...

le mutuz le nation,le mzee watotoz mother Fanta na mother cocacola.
nataka kujua una degree ngapi umezipata kutoka new York city na ni vyuo ghani na degree hizo umesomea nini?au umesomea ubaharia kama ulivyosema mwenyewe ulikuwa unaupenda.

na Belgium umesomea nini? nitashkuru kama ukinijibu maswali yangu mkuu.natanguliza shukran na heshma kwako kubwa.