
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania unakutaarifu Harambee ya kukusanya pesa kwaajili ya kusaidia kuandaa semina ya kuwaelimisha Wabunge wa Bunge la katiba umuhimu wa raia pacha kama wewe ni mkereketwa wa hili swala na usiku haulali linakufulukuta na hii ni kwa faida yako na vizazi vyetu vijavyo hata kama wewe hautalifaidi, kufika kwako kwenye harambee hii utakuwa umewajengea watoto wako msingi mzuri wa DUAL CITIZENSHIP.
Hii ni haki yako lazima upiganie hata kama watu wengine hawaoni umuhimu wake ni kwa sababu ya kutoelewa na kujisahau hata kama utajichubua ufanane na mzungu asili yako itabaki Mtanzania, wewe umezaliwa Tanzania, umekulia Tanzania, umesomea Tanzania ni Mtanzania halisi kwa nini uwe mgeni kwa nchi ya watu wakati una nchi yako Tanzania?
Fikiri kwa makini uraia uliopewa na nchi nyingine ni wa makaratasi tu siku wakikunyang'anya utaenda wapi wakati nchi yako ulikozaliwa inakukataa kwa sababu ya hilo karatasi ulilopewa kwa ajili ya maisha ya ughaibuni yawe nafuu. kumbuka ughaibuni sio nchi yako, Tanzania ndiko ulikozaliwa daima utaipenda Tanzania na siku zote utabaki kuwa Mtanzania asilia.
Harambee itafanyika kesho Jumapili March 23, 2014 Meadowbrook park address ni 7901 Meadowbrook lane, Chavy Chase, MD 20815
Jumiya DMV itachoma nyama huku tukifanya harambee
Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.
MIMI NI MTANZANI, NIMEZALIWA TANZANIA, NIMEKUILIA TANZANIA, NAISHI UGHAIBUNI NDIO MAANA NASEMA URAIA PACHA NI HALALI YANGU NA HAKI YANGU YA MSINGI.
14 comments:
Kwanza kabisa, naunga mkono hoja ya uraia pacha.
Swali langu nalielekeza kwa viongozi wetu wa jumuiya za Watanzania. Je, akaunti za Jumuiya hazina pesa mpaka tuanze kukusanya dola kumi kumi kutoka kwa mtu mmoja mmoja kwa swala muhimu kama hili? Kama jibu la swali langu ni kwamba akaunti hazina pesa, then please consider this to be the end of my post. Otherwise, endelea hapa chini.
Kwa USA pekee yake, kuna jumuiya za Watanzania zaidi ya kumi. Kwa maana hiyo, kama akaunti ya kila jumuiya ikichangia $2,500 tu tayari tutakuwa tumeshapata ile pesa inayohitajika kwa shughuli hii. We gotta be serious about our special interests before others can take us seriously. Inahuzunisha kwamba every now and then tumekuwa tukizitumia akaunti hizi kulipia gharama za recreational activities, lakini sasa hatuwezi kuzitumia kwa shughuli muhimu na nyeti kama hii.
Kama kazi ya akaunti za jumuiya ni kuendeshea party, basi hizo akaunti hazihitajiki kwa sababu wanajumuiya wanao uwezo wa kujilipia kushiriki kwenye parties wazozitaka.
Hio pesa ya nyama mimi naona muiongezee lwenye michango.asanteni.mdau
Kweli nyie wapumbavu nimeona ni wajinga kujichubuwa inausiana vipi na duo kweli nyie ni wajinga na hamna hoja yani kujichubuwa ndiyo mmeona point ya kuita watu mmeshashindwa na mmedharaulika uswahili mmeshaweka
tatizo hao wabunge wenyewe ni mafisadi wanakula laki tatu kwa siku ,na sisi brother unajua mazingira yetu ya kupata hela huku kama wao wana ubinadamu watusaidie tu bila mchango wowote
Warioba Draft March 19, 2014
Watanzania tuniko ugaibuni na wale walioko nchini Tanzania, tuangalie hisi sehemehu kwa makini- "Crtical thinking" ili tupate kuelimishana wote kwa kaya masuala ya Uraia wa nchi mbili. Wanaosema hapana au ndiyo wanakaribisha kutoa maoni yao wakiwa na ushahidi- supporting scienfic evidence.
Uraia
42. Uraia ni msingi wa utambulisho (identity) unaompa raia haki ya kulindwa na nchiyake, ikiwa ni pamoja na haki zake za binadamu za asili na zisizoondosheka(inherrent and inalienable rights) kama zilivyotambuliwa au zitakavyotambuliwa
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba za Nchi Washirika na Mikataba ya Kimataifa.
43. Uraia kama ulivyowekwa katika Rasimu ya Katiba, umejengwa katika msingi wauzalendo usiotiliwa shaka (patriotism) unaompatia raia wajibu wa kuitetea, kuilindana kuifia nchi yake bila ya mashaka. Kwa hiyo, Uraia ndiyo kigezo na sifa yakupewa dhamana ya uongozi wa Taifa na kuajiriwa katika mihimili ya Serikali na vyombo vya Ulinzi na Usalama. Rasimu inapendekeza kutambuliwa kwa uraia wakuzaliwa na uraia wa kujiandikisha ambao, katika kujidhihirisha kwake, ni uraiawa nchi moja usiojenga au kuleta hisia za kuwabagua au kuwatenga raia katikamatabaka na madaraja yanayotokana na tofauti ya hali au fursa zao.
44. Rasimu ya Katiba pia inapendekeza kuwapatia hadhi mahsusi watu wenye asili aunasaba ya Utanzania ambao wameacha kuwa raia wa Tanzania kwa kuchukuaUraia wa nchi nyingine.
45. Lengo ni kuwarahisishia watu wenye asili ya Tanzania waliochukua uraia wa nchinyingine wakija hapa nyumbani Wasipate usumbufu usio wa lazima na pia iliwarahisishiwe ushiriki wao katika ujenzi wa taifa kwa kuwawezesha kuchangiaipasavyo katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Utaratibu kama huuunafuatwa katika nchi kadhaa, kwa mfano Ethiopia, India na Ujerumani ambako umeonyesha mafanikio.
Temba
Namuunga mkono mdau wa 12:44PM. Hili suala ni letu wote,tunaelewa umuhimu wake. Haina haja kumvuta mtu na nyama choma, na kama ikichomwa iuzwe kuongezea michango.Ni maoni tu.
MBONA HAMJAVAA RANGI ZENU ZA CCM?
Huyu mtu juu anechukia kuhusu mtu kujichibua kwasababu na yeye anafanya. Back to the subject. Hili ni neno lizuri na tunawahunga 100%
Wadau, nadhani wengi tumeelimika hapa Marekani. Sisi wenye uraia hapa tuliuchukua kwa hiari yetu, baada ya kuukanusha UTanzania. Tunao uwezo wa kuukana huu uraia wa hapa na kuurudisha Utanzania. Hivyo vitisho vya kutuambia kuwa lazima tuchangie ni wazimu tuu. Mnasema kuwa kama Mtu akinyang'anywa Makaratasi atakwenda wapi? Tanzania haitakukana ukitaka kurudi. Pigia ubalozi watakufafanulia kwamba hutaadhibiwa kuurudia uraia wako.
Jamani, acheni kukerwa na hili suala la uraia pacha. Contributions are relevant when they are for great causes and dual citizenship is not one of them!
Wapendwa Watanzania wenzangu mimi ni MTanzania ninaeishi UK,na pia muumini mzuri wa URAIA WA NCHI MBILI, naomba msiwe na "JAZBA"mpaka kuitana wajinga si usitaarabu wala utamaduni wetu,nanyi viongozi wa jumuiya jaribu kutumia hoja na ushawishi wenye kauli nzuri na heshima kuwashawishi watanzania wenzenu wa USA waje kwenye kikao na kufanya harambee, kauli za kwamba hata "UKIJICHUBUA "vipi utabaki kuwa mtanzania si kauli nzuri wala za kupendeza kwa dada zetu,siungi mkono swala la kujichubua lakini hiyo ni hiari ya mtu mwenyewe ili mradi havunji SHERIA za nchi husika ni maelizie kuwa hekima na busara vitawale kwetu sisi watanzania tuishio ughaiuni,natumai harambee yenu itakwenda vizuri
NB Wakazi wa uk na vitongoji vya jirani tunamsubiri BWANA MKUBWA takuja hapa tarehe 30 March na ataongea na watanzania
MUNGU IBARIKI TANZANIA, NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA
Mimi pia naunga mkono raia pacha kwasababu hivi karibuni nategemea kupata kipande cha kazi---excited and can't wait! Kwa maana nyingine mimi sijaukana utz. Baada ya huo utangulizi napenda kusema kuwa swala la raia pacha kwa sasa ni gumu/haliwezekaniki kwasababu zifuatazo:
[1]. Kuhusu Funds. Hakuna na haitapatika pesa kamwe ya kutosha kuwalipa au kulobby wabunge ili wapitishe hiyo bill. Mfano wa karibuni: wabunge maalumu wa rasimu ya katiba mpya wanalipwa about 300K/day, lkn about a month ago, baadhi yao walilalamika kuwa haitoshi na wanahitaji nyongeza, imagine!!!!! Sana sana ninacho kiona hapa: Jumuia itakusanya hela, months later itakuja kulaumiwa kuwa imekula hela ya watu. Wakati huo viongozi waliyopo hawatakuwa tena madarakani na jina la jumuia linaachiwa doa la wizi. Msisahau kuwa, Jumuia bado haipokelewi kihivyo na wana DMV walio wengi---has something to do with previous experience.
[2]. Elimu na faida ya raia mbili. Faida ya raia pacha na elimu yake haipo kwa watanzania waishio Tanzania (siyo wa ughaibuni). Watanzania wa Tanzania wakielemishwa kupitia media za kila aina faida ya raia pacha, then watakuwa na mwamko na eventually wabuge watapata attention kutoka wananchi walio wachaguwa na hopefully swali zima la raia pacha litapata attention.
[3]. Raia pacha si muhimu kwa JK. Kwasababu raia pacha haikuwahi kuwa platform ya JK wakati anagombea uraisi na hata reelection yake, raia mbili siyo priority kwake na hawezi kuipush hard, na pengine mpaka anaondoka ofisini, unfortunately! Again (refer item #2), constituencies na priority ya JK ni watanzania waliomchagua na waishio tz. Haoni tija kwake kuhangaika na Watanzania waishio nje ya nchi (they don't vote and therefore no consequences).
*****Mwisho, tunaweza kutofautiana hoja/approach bila matusi au jazba*****
~edward~
Wakati ukuta lilipitishwa 1964 na bunge kuwa hakuna haja kuwa na uraia pacha miaka hamsini iliyopita kwani watanzani wakiokuwa nje ya nchi walikuwa wachache.
Sasa typo wengi tulikuja ughaibuni kutafuta maisha na elimu kwetu na vizazi vyetu
Tuwe na upeo wa kuangalia kesho na keshokutwa kwani ukoloni unarudi kwa namba nyingine kuchukua mashamba mashirika mashule viwanda kwa visingizio vya kuwekeza tukiwa na uraia pacha tutawekeza pamoja kwani tumesha wagundua. Tuamke tusije baki nyuma kwa miaka mingine hamsini
Mungu ibariki Tanzania na ufanikishe jambo hili la uraia pacha ili kuleta maendeleo ya kweli katika nchi yetu
makaratasi ya hapa marekani tunayo!Tanzania bado nchi change sana, wananchi bado awajajitambua vizuli! kwa iyo awajui bado umuihim wa uraia pacha, kwa maoni yangu tujadili tutapata vipi makaratasi ya hapa USA !
Kweli nguo za CCM ziko wapi? Viongozi wa CCM wanasupport hii dual system kwasababu watoto wao ni raia wa nchi nyingine. Janga la taifa.
Post a Comment