Advertisements

Friday, July 24, 2015

Madaktari kutoka Washington Diaspora Walioletwa na Jumuiya ya Watanzania DMV Watoa Hudua ya Afya Hospitali ya Mnazi Mmoja

Dr Nofali akizungumza na Ujumbe wa Madaktari kutoka Washington Diaspora walipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kutoa huduma ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Tiba ya Meno ukiwa na Ujumbe wa Watu 17, Wamefika Ofisi hapo kujitambulisha kwa Uongozi wa hospital 
Dr Nofali akizungumza na Madaktari hao walipofika Ofisini kujitambulisha wakiwa na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Diaspora Zanzibar Ukiongozwa na Mkurugezi wa Idara hiyo Ndg Adila 
Ujumbe wa Madaktari Madiaspora wakimsikiliza Dr Nofali walipofikac Ofisini kwakwe kujitambulisha na kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata tiba.
Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Washington Diaspora Asha Nyanyanyi akiztowa maelezo ya Ujumbe huo kwa Dr Nofali wakati walipofika Ofisini kwake Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja leo asubuhi kwa kutoa huduma za Meno Kisukari kutoa dawa kwa wagomjwa na kutowa elimu ya Saratati ya Matiti kwa Wanawake Zanzibar na kupima 
Madaktari Diaspora kutoka Washington wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo kujitambulisha kabla ya kuaza kutoa huduma kwa wagonjwa. 

1 comment:

Anonymous said...

Natoa pongezi kwa uongozi wa watanzania wa DMV kwa kusaidia nyumbani. Ni mambo kama haya yatapunguza ufa uliopo baina ya watanzania walioko nje na wale waliopo nyumbani na hivi kuonesha kuwa tuko pamoja "despite being far from one another - distance wise."