Kampuni ya bigright promotion inategemea kuandaa pambano la masumbwi litakalopigwa tarehe 6/9/2015 katika ukumbi wa vijana , kinondoni
Katibu wa ngumi za kulipwa na ndie mratibu wa mpambano huo Ibrahim kamwe (bigright) alisema pambano hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuamsha vijana kujituma kujijengea mazingira ya kupenda kufanya kazi sio kukaa vijiweni na kujiingiza katika utumiaji wa madawa na ukabaji , bigright promotion ikishirikiana FRIENDS OF DEVELOPMENTS (FOD) yaani rafiki wa maendeleo wanaandaa pambano hilo kwa kuwachezesha mabondia toka sehemu tofauti za Tanzania
Mbena Rajabu atazipiga Twalibu mchanjo katika pambano la ubingwa wa taifa kilogram 57. Dula mbabe atazipiga na ambukile chusa, haidary raju atapambana mtango salum kutoka tanga,yona miyeyusho atazipiga na hemedi hemed,huku George alen wa tanga akizipiga na mwinyi mzengela wa daresalaam.mau champion wa tanga atazipiga na Epson john wa morogoro.mohamed alkaida na guzo Hassan.lengo la FoD kushirikiana na bigright katika kuandaa pambano hilo ni kuhakikisha Tanzania tunakuwa na mabingwa wengi wa ngumi katika mikoa yote,na kuhakikisha wanamichezo wengine na wasanii wanafanya vizuri katika fani zao,kwa kuwa FOD ina wafuasi kila kona ya Tanzania imelenga kupigana vilivyo kuhakikisha majiji yanakuwa safi wasanii na wanamichezo wanafika mbali kuwasaidia wasiojiweza mitaani na mahospitalini.
Kwa ufupi litakuwa ni pambano la aina yake kutokana na hao mabondia wenyewe kuwa na uchu wa ushindi na ni mabondia wazuri wazoefu na wana wapenzi wengi.
No comments:
Post a Comment