MBUNGE MBATIA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA KIJIJINI KWAO KWAMARE JIMBONI VUNJO.
Mbunge wa kuteuliwa,Mh James Mbatia akiwasili katika kijiji cha
Kirua Vunjo Magharibi na kupokelewa na msaidizi wake Hamis Hamis kwa
ajili ya zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
kupitia BVR.
Mbunge wa kuteuliwa ,Mh James Mbatia akisalimiana na wananchi mara
baada ya kuwasil katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua Vunjo Magharibi
Jimbo la Vunjo kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura.
Mbunge James Mbatia akitoa maelezo yake kwa mmoja wa maofisa wa
zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kupita
mfumo wa BVR.
Mbunge James Mbatia akichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la
uandikishaji katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua
Vunjo.
Mh Mbatia akitia saini katika kifaa kimoja wapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.
Mh Mbatia akiweka vidole gumba kwa ajili ya kuchukuliwa alama.
Afisa uandikisha akimkabidhi Mh Mbatia kitamburisho chake mara
baada ya kumaliza zoezi la
uandikishaji.
Mh Mbatia akionesha kitamburisho maalumu kwa ajili ya zoezi la
kupiga kura litakalofanyika hapo baadae mwezi
oktoba.
Msaidizi wa Mh Mbatia ,Hamis Hamis akikabidhiwa kitamburisho chake
mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu
la wapiga kura. Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment