MKUTANO maalumu wa maendeleo na kutokomeza Maralia Barani Afrika umeanza rasmi leo Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huo ulioanza rasmi leo, unatarajia kumalizika Julai 16 mwaka huu na unalengo la kujadili mikakati ya kuzikwamua nchi maskini kwa kuzichangia kimaendeleo nchi zenye uhitaji maalumu hasa kijamii kutoka kwa asilimia watakayokuwa wamekubaliana ili kutokomeza umaskini.
Akizungumza na wanahabari Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa UN, Stella Vuzo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama zinazojumuika katika mkutano huo wa nchi za bara la Afrika ambayo inahitaji kuinuliwa kuichumi.
Amesema kuwa mawazo na matokeo yatakayo jadiliwa kwenye mkutano huo yatasaidia kuziwezesha nchi zenye mahitaji ya kujikwamua kiuchumi ili kuweza kufikia malengo watakayokuwa wamekubaliana likiwemo la kutokomeza ugonjwa wa Maralia kwa zaidi ya miaka 15 ijayo kuwa umeisha.
“Malengo na mawazo yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo yataziwezesha nchi hitaji kujikwamua kuichumi na kimaendeleo kwani zitawezeshwa asilimia fulani ambayo watakubaliana kuzichangia kwenye kikao hicho,” alisema Stella.
(NA DENIS MTIMA/GPL)
No comments:
Post a Comment