Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika DRC Bw. Martin Kobler akiwasilisha taarifa mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu, hali ya usalama na mkakati wa kupunguza walinzi wa amani. na Kueleza kwamba utekelezaji wa mamlaka ya MONUSCO unahitaji ushirikiano endelevu kati yake na mamlaka za DRC
Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwanzo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Dina Kawar akiwasilisha taarifa ya Kamati yake mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambapo pamoja mambo mengine ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkamata na kisha kumpeleka nchi Uganda kiongozi la kundi la wanamgambo la Allied Democratic Forces ( ADF) Bw. Jamil Mukulu ambaye alikuwa katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Kamati hiyo.
Na Mwandishi Maalum , New York
Uwezo wa Misheni ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) wa kutekeleza mamlaka yake kikamilifu utategemea zaidi ushirikiano na uhusiwano wake na mamlaka za nchi hiyo.
Hayo yameelezwa na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika DRC, Bw. Martin Kobler wakati alipowasilisha taarifa yake mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya jumaane.
Taarifa Bw. Kobler kwa Baraza hilo ilihusu maeneo matatu ambayo ni uchaguzi mkuu utaotarajiwa kufanyika mwakani, hali ya usalama na mkakati wa upunguzaji wa idadi ya walinzi wa Amani.
“ Mafanikio ya utekelezaji wa mamlaka yetu unategemea na kuendelea kwa majadiliano na ushirikiano na serikali na hususanu kuhusu hali ya usalama katika eneo la Mashariki na Mchakato wa Uchaguzi.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, ameliambia Baraza kwamba, kuna matumaini katika baadhi ya maeneo. Akibainisha juu ya operesheni zinazoendelea dhidi ya kundi la wanamgambo la Force de Resistance Patriotique en Ituri ( FPRI) na zinazofanywa na Jeshi la DRC ( FARDC) kwa kusaidiwa na MONUSCO.
“ Wakati kipaumbele ni kuhakikisha kuwa kundi hili linasalimisha silaha kwa hiari, matumizi ya nguvu ilibidi yafanyike baada ya kunvujwa mara tatu muda wa mwisho ambao kundi hilo lilipashwa kusalimisha silaha zake kwa hiari” amesema Bw. Kobler
Kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya kundi la Force Democratique de Liberation du Rwanda ( FDLR) katika maeneo ya Kivu Magharibu, Kivu ya Kusini na Katanda amsema operesheni hiyo imesimama kwa zaidi ya miezi mitano.
Amefafanua kuwa kusimama kwa operesheni hiyo ambayo ilitakiwa ifanywe na FARDC kwa kusaidiwa na MONUSCO licha ya kwamba pamoja na mambo mengine kulitoka na hoja ya awali kuhusu haki za binadamu bali sasa limekwenda mbali zaidi ya hapo.
Akaongeza kwamba wakati MONUSCO ikirejea na kufanya tathmini kuhusu haki za binadamu ilikuwa inatafuta njia ya namna ya kuendeleza ushirikiano kupitia mpango uliopo sasa.
Akielezea zaidi kuhusu hali ya usalama, Bw. Martin Kobler amesisitiza kuwa wakati serikali ya DRC imepiga hatua kubwa katika kurejesha hali ya Amani katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Bado wananchi wa eneo la Mashariki ya nchi hiyo maisha yao yanategemea sana huruma ya makundi ya wanamgambo wenye silaha.
Pamoja na mafanikio ya kupunguza nguvu ya FDLR katika baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyakalia, jeshi la DRC limejikuta katika mazingira magumu ya kuyadhibiti na kuyashikilia maeneo yaliyokombolewa na kwamba hakuna muda wa kusubiri.
Kuhusu uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2016, Bw. Kobler amesema wajibu wa kuhakikisha kwamba uchaguzi huo unakuwa wa huru, haki na wazi ni wa serikali yenyewe ya DRC
Akaongeza kwamba tajio la haraka katika kuhakikisha kwamba uchaguzi utafanyika kwa wakati ni fedha , kalenda sahihi ya uchaguzi, uboreshaji wa daftari la wapiga kura na utoaji wa fursa kwa vyama vya upinzani. Akamsifu Rais Kabila kwa kupanua wigo wa majadiliano na wadau mbalimbali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.
Katika hatua nyingine. Mwakilishi wa Jordan na ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwanzo dhidi ya DRC, Dina Kawar , ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumkamata na kisha kukubali kumpeleka nchini Uganda kiongozi wa Kundi la Allied Democratic Force ( ADF) Bw. Jamil Mukulu
Ametoa shukrani hizo wakati naye alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Kamati yake mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa


No comments:
Post a Comment