Wednesday, July 8, 2015

MSHINDI WA TUZO YA BET, EDDY KENZO ALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE NCHINI UGANDA

Eddy Kenzo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe.
Mashabiki wa Kenzo wakimlaki kwa shangwe.
Kenzo akilia machozi ya furaha wakati wa mapokezi hayo.
Ilikuwa ni shangwe ndani ya Entebbe.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza wakati wa mapokezi hayo.
Mashabiki wakifurahia tuzo hiyo.
Mapokezi hayo yakiwa yamepamba moto.
Eddy Kenzo baada ya kutwaa tuzo yake nchini Marekani.

MWANAMUZIKI wa Dancehall nchini Uganda, Edrisa Musuuza maarufu kwa jina la Eddy Kenzo, amewasili nchini humo jana akitokea Marekani aliposhinda tuzo ya BET ya Chaguo la Watazamaji (Viewer's Choice Award).

Mashabiki lukuki wa mwanamuziki huyo jana walifurika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kumpokea staa huyo aliporejea kutoka nchini Marekani.

Staa huyo wa wimbo wa Sitya Loss aliwasili saa 3:30 alasiri na kupata mapokezi ya kishujaa akiwa ndiye mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kutwaa tuzo hiyo.

Kenzo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwabwaga Cassper Nyovest wa Afrika Kusini, George the Poet na MiC LOWRY wa Uingereza, MzVee wa Ghana na Novelists kutoka Ufaransa aliokuwa akishindana nao katika kipengele cha Tuzo ya Chaguo la Watazamaji.\\

Credit GPL

No comments: