JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI (Jeshi la Magereza) |
||
Anwani ya
Simu :" MAGEREZA"
Simu
namba: (+255) - 022 : 2110314-6
Fax:
(+255)-022: 2113737
Email:cgp@prisons.go.tz
TOVUTI:
www.magereza.go.tz
|
|
OFISI
YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA,
S.L.P. 9190,
DAR ES SALAAM.
|
MAFANIKIO YA JESHI LA MAGEREZA KATIKA KIPINDI CHA
SERIKALI
YA AWAMU
YA NNE (MWAKA 2005 - 2015)
1.0 UTANGULIZI
1.1.0 Historia ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara
Jeshi
la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25, 1931, Dhima yake kuu ni
kuchangia ipasavyo katika kuimarisha usalama wa jamii kupitia usimamizi wa
kifungo na huduma za mahabusu, utekelezaji wa program za urekebishaji wa
wahalifu na kutoa ushauri wa kisera kuhusu uzuiaji wa wahalifu.
·
Majukumu
na malengo ya Jeshi la Magereza
Jukumu
la msingi la Jeshi la Magereza ni kuwahifadhi wafungwa na mahabusu wa aina zote
na jukumu la urekebishaji wa tabia za wafungwa pia hufanyika kupitia program za
mafunzo kwa njia ya vitendo katika miradi ya kilimo, viwanda vidogo vidogo na
ujenzi. Vile vile, ushauri nasaha hutolewa kwa wafungwa kwa kutumia waalimu wa
dini na maafisa ustawi wa jamii pale inabainika kuhitajika kulingana na hali ya
mfungwa husika.
2.0 MAFANIKIO
·
Katika utekelezaji wa majukumu yake
katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nne mwaka 2005 hadi 2015 Jeshi limepata
mafanikio katika maeneo makuu kama
yafuatayo:-
·
Uimarishaji
wa Magereza yenye Ulinzi Mkali (Central Prison)
Mfano
ukarabati wa majengo na uboreshaji wa miundo mbinu ya Magereza yenye ulinzi
mkali umefanyika katika Magereza ya Butimba, Uyui, Lilungu, Maweni, Isanga,
Keko na Ukonga.
·
Ujenzi,
ukamalishaji, upanuzi wa majengo ya Ofisi
Mfano,
Ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Magereza Mikoa ya Singida, Ofisi ya Magereza Mkoa
wa Dar Es Salaam unaendelea na ukarabati wa Jengo la Makao Makuu ya Magereza
lililoanza rasmi kutumika Desemba 31, 2007.
·
Ujenzi
wa nyumba za askari
Mfano,
ghorofa la kuishi askari takribani familia 16 mkoani Iringa, ujenzi wa nyumba
za maofisa na askari unaendelea kufanyika katika Magereza mbalimbali nchini.
·
Maji
safi na maji taka Magerezani
Uimarishaji
wa miundombinu ya maji safi umefanyika katika Magereza ya Kwamngumi, Kambi
Kimbiji, Kikosi Maalum (KMKGM), kambi Chikuyu, Segerea na sehemu zingine
unaendelea.
·
Kupunguza
Msongamano Magerezani
Jeshi
la Magereza katika jitihada za kupunguza msongamano Magerezani limefanikiwa
kuongeza uwezo wa magereza kutunza wahalifu kutoka nafasi 22,699 zilizokuwapo
mwaka 2005 hadi nafasi ya 29,552 zilizopo sasa. Ongezeko hili la nafasi za
kulala wafungwa 6,853 ni sawa na asilimia 30.2 ya nafasi zilizokuwepo kabla
mwaka 2005.
·
Kuimarisha
Viwanda vidogo vidogo
Jeshi
la Magereza limeendelea kuimarisha
Viwanda vidogo vidogo kwa kuendelea na ufungaji wa mashine katika karakana ya
Uhunzi Ukonga, kiwanda cha viatu Karanga Moshi, nakadhalika.
·
Kuimarisha
Mashamba ya Kilimo na Mifugo
Jeshi
la Magereza linahudumia ng’ombe wa nyama, wa maziwa pamoja na Mbuzi, Kondoo,
Nguruwe, Sungura, Kuku wa mayai na Bata weupe. Aidha, Jeshi la Magereza lina
mashamba ya mbegu bora za kilimo kwa
kushirikiana na Wakala wa Mbegu za Kilimo nchini Agricultural Seed Agency (ASA) katika mikoa ya Arusha, Dodoma,
Manyara, Lindi, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Morogoro.
·
Matumizi
ya Nishati mbadala Magerezani
Jeshi
limeendelea na juhudi zake za kupunguza matumizi ya kuni na badala yake kutumia
nishati mbadala kama vile gesi itokanayo na tungamotaka (Biogas) na Makaa ya
mawe kwa upikaji wa chakula cha wafungwa.
·
Mafunzo
mbalimbali
Mafunzo
mbalimbali yaliendeshwa ndani ya Jeshi
la Magereza na watumishi 7,683 walihitimu kozi mbalimbali, kwa upande wa
mafunzo katika vyuo vya nje ya Jeshi watumishi 519 wamehitimu masomo ya taaluma. Aidha, watumishi wa kada mbalimbali
wapatao 169 wamepata fursa ya kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo
mbalimbali au kushiriki kwenye vikao vya kimataifa.
·
Usafirishaji
Mahabusu
Jeshi
limepanua utekelezaji wa jukumu la kuwapeleka mahabusu Mahakamani kusikiliza
kesi. Zoezi hilo lilianza rasmi tarehe 19 Mei, 2008 kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kwa sasa zoezi hilo
linaendelea katika Mkoa wa Arusha na baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma.
·
Utoaji
wa Huduma za Afya
Kwa
kushirikiana na Shirika la PharmAccess International, New life in Christ na
baadhi ya Halmashauri hapa nchini tumefaninikiwa kujenga Zahanati na Vituo vya
Afya katika mikoa Ishirini (20).
·
Kuwawezesha
askari na watumishi kupambana na umaskini
Jeshi
limeendelea na mchakato wa kufungua Maduka ya Bidhaa zisizolipiwa kodi (Duty
Free Shops) ili kupunguza makali ya maisha kwa watumishi wa Jeshi la Magereza
na familia zao. Maduka ya aina hii yamefunguliwa Ukonga – Dar es Salaam, Gereza
Isanga – Dodoma, Gereza Karanga – Moshi, Chuo KPF – Morogoro, Gereza Butimba –
Mwanza, Gereza Ruanda – Mbeya, Gereza Keko na Gereza Uyui – Tabora.
·
Uhifadhi
wa Mazingira
Hadi
kufikia Aprili, 2015 miti 4,321,450 imepandwa nchi nzima na katika Miradi
maalumu inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali kwa mfano UNDP/NORAD ikishirikiana
na Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Tanzania Forestry Fund (TFF) katika magereza ya Isupilo, Msalato,
Idete, Mgagao, Kambi Mkwaya, Kambi Ihanga.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
8 Julai, 2015
No comments:
Post a Comment