Wednesday, July 8, 2015

MZEE KINGUNGE ATOA YAKE YA MOYONI MJINI DODOMA LEO

MWANASIASA mkongwe nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Julai 8, 2015, Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’, alionya

Amesema, CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.

“kuna kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema Mzee Kingunge.
"CCM lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye uchaguzi".

Hivi karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.

Hata hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao vya chini.

5 comments:

Anonymous said...

TATIZO LA Mzee wetu huyu Kingunge Ngombale wa Mwilu anaonekana kuibomoa heshima yake aliojijengea kwa miaka mingi ya utumishi katika Chama na serukalini kwa kutuwa mkweli baadala yake amekuwa yupo katika kambi ya Mh.Lowassa ,kwa maana hiyo mzee Kingunge amekuwa mwenye upendeleo na mtetezi wa Lowassa ,hana hoja ya msingi hata kidogo bora awawachie viongozi wa juu wa CCM wafanye kweli

PETRO said...

Huyu mzee nae siapumzike Kama wenzie ?

Anonymous said...

Mzee Kingunge, umeshakula mtaji wako wa kisiasa kwa kufungamana na kambi ya kada mmoja wa chama chako. Kwa sasa mgongano wa maslahi unakutafuna na hakuna ushauri unaoweza kuutoa kwa CCM ukatiliwa maanani kama ushauri kutoka kwa veteran wa CCM.

Anonymous said...

Shika adabu wewe Anonymous July9,2015 at 12:56am Diaspora community haina mtia nia na for your information the majority of diaspora community are not interested na siasa za malumbano..

Anonymous said...

Huyu Mzee ndio mwanzo wa matatizo yoote tunayoyaona nchini. Hebu nipatieni email yake aka kama anayo. Lol!
Bora enzi za Kawawa walikuwa na uungwana, huyu ni fashisti na wala sio fisadi.