Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Baadhi ya vigogo wa serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na waliokuwa baadhi ya wabunge wa majimbo nchini, jana walijikuta wakipigana vikumbo katika ofisi za chama hicho kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania ubunge katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Chama hicho kutangaza kuanza kutoa fomu hizo jana kwa wanachama wake wanaotaka kuteuliwa na chama hicho kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini kwenye uchaguzi huo utakaovishirikisha vyama vingi vya siasa nchini.
Ni baada ya kukamilisha mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Dk. Ali Mohamed Shein kwa Zanzibar katika vikao vya chama hicho vilivyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
NAPE ACHUKUA FOMU
Nape jana alikuwa miongoni mwa wanachama wanane wa CCM waliokabidhiwa fomu za kuwania ubunge katika majimbo matatu ya Wilaya ya Lindi likiwamo la Mtama baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe kabla ya Rais Jakaya kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni baada ya wabunge kumaliza kipindi chao cha miaka mitano. Hata hivyo Membe alitangaza hatagombea tena katika jimbo hilo baada ya kutangaza nia yake ya kukiomba chama hicho kumteua kugombea urais Oktoba 25, mwaka huu.
Wengine na majimbo hayo kwenye mabano ni Bakari Said Maguo; Masoud Ally Mikorogo na Ibrahimu Kadhi Ibrahimu (Lindi Mjini), Yusufu Amani; Adamu Kulagwa na Dk. Alawi Mikidadi (Mchinga).
Makatibu wa CCM Mohamedi Kateva (Wilaya ya Lindi Mjini na Christina Gukwi (Lindi Vijijini) wamethibitisha wanachama hao kuchukua fomu hizo jana.
ZUNGU, IDD AZZAN WAMO
Uchukuaji wa fomu hizo katika mkoa wa Dar es Salaam umeonekana kuwa na mwitiko mkubwa kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuchukua fomu hizo.
Kati ya watu waliofungua dimba la kuchukua fomu kwa wilaya ya Kinondoni ni Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Idd Azzan, ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua fomu hiyo.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Azzan, alisema ameamua kutetea jimbo lake kwa mara nyingine ili amalizie kusukuma maendeleo aliyoyaanza.
Mwingine ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki, ambaye amechukua fomu ya kugombea ubunge wa viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM, kupitia wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam.
WAKILI KUGOMBEA KAWE
Kwa upande wa Jimbo la Kawe, mpaka NIPASHE linakwenda mitamboni, walikuwa wamechukua fomu wagombea saba, akiwamo Wakili, Jumaa Mhina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Jamii ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM).
Mhina alisema kuwa amechukua fomu ya kuwania ubunge ndani ya chama hicho kwa mara nyingine jana baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha mwaka 2010 ndani ya chama hicho.
Alisema lengo ni kuhakikisha analirudisha jimbo la Kawe CCM kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kwa upande wa waliojitokeza kwa jimbo la Ubungo walikuwa wawili, Kinondoni wawili na Kibamba wawili.
Kwa upande wa ubunge viti maalum kupitia UWT wilaya ya hiyo, wanachama ambao walikuwa wamechukua fomu mpaka muda huo ni 11 na madiwani 15.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wilaya hiyo, Athuman Shesha, alisema fomu zinatolewa kwa kila mgombea kulipia Sh. 100,000.
SILAA, MTEMVU
Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale, aliwataja waliochukua fomu hizo kwa majimbo ya Ukonga kuwa ni aliyekuwa Meya wa Ilala, Jerry Slaa, Jacob Kasema, Hamza Mshindo na Fredrick Rwegasira.
Segerea: Zahoro Lyasuka, Apruna Jaka, Bonna Kalua na Ilala ; Musa Azzan maarufu kwa jina la Zungu.
Temeke: Katibu Msaidizi wa Wilaya Wilaya ya Temeke Yona Sengelema, aliwataja waliochukua fomu kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Abbas Mtemvu, Mama Maimuna na Maimuna Kayanda; Joseph Mhoha.
Kigamboni: Haroun Othman
Mbagala: Mindi Kuchilingula, Lucas Malegeli, Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC Taifa), Kazimbaya Adeladius.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu- Umoja wa Wanawake Wilaya ya Temeke (UWT), Fatuma Manyanga, alisema wanachama 15 walichukua fomu za kugombea ubunge wa viti maalum akiwamo Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Back to Life, Pilli Misana aliyechukua fomu kugombea ubunge viti maalum kupitia taasisi hizo (NGO’s).
Naye; Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanawe, kinachomiliki Bendi ya Yamoto, na kiongozi wa Kundi la TMK wanaume, Said Fella, amechukua fomu ya kuwania udiwani katika kata ya Kilungule iliyopo Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Saalam. Fella alisema ameamua kugombea udiwani ili aweze kutatua kero za wakazi wa kata hiyo na kuwaletea maendeleo.
RAIS SHIRIKISHO LA MUZIKI
Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Muziki Nchini, Ado Mwasongwe, amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuomba kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini kupitia CCM.
Mwasongwe katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 aliweza kuomba nafasi hiyo lakini kura hazikutosha.
MGAYA WA TUCTA
Katibu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya, amechukua fomu kuwania ubunge katika Jimbo la Muheza mkoani Tanga na kummwagia sifa Waziri wa Ujenzi, John Magufuri kuwa anafaa kuongoza nchi kwa kuwa ni jembe kutokana na uchapaji kazi wake.
Mgaya alimmwagia sifa hizo Magufuli jana baada ya kutangazwa na CCM kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu.
Akizungumza kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Muheza, wakati akichukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Muheza, alisema kila Mtanzania anafahamu utendaji kazi na misimamo ya Magufuli katika wizara alizopewa kuziongoza kwa lengo la kuliletea taifa maendeleo.
Fomu hiyo alikabidhiwa na Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya hiyo, Tija Magoma majira ya saa 4 asubuhi.
NYENYEMBE AMVAA TENA SUGU
Mwandishi Mwandamizi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima mkoani hapa, Christopher Nyenyembe, amejitosa kwa mara nyingine kuwania ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lililokuwa linaongozwa na Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu wa Chadema.
Nyenyembe jana alichukua fomu katika ofisi za Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, kisha kuwaelezea waandishi wa habari kuwa anataka kuwatumikia wananchi wa Mbeya na kuwakomboa kiuchumi.
Alisema ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi mwenye uwezo wa kuwatumikia wananchi kujitokeza kugombea uongozi kama alivyofanya yeye.
Katika kura za maoni ndani ya chama hicho mwaka 2010, Nyenyembe alikuwa mshindi wa tatu akitanguliwa na Mponzi aliyekuwa wa pili wakati Sugu akifanikiwa kupitishwa, hatimaye kupeperusha bendera ya Chadema na kuipatia ushindi.
SILINDE ATIMKIA MOMBA
SIKU chache baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutangaza majimbo mapya 26 ya uchaguzi Tanzania Bara, aliyekuwa Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde, ametangaza kuachana na jimbo jipya la Tunduma na kwenda kugombea katika jimbo la Momba.
Katika mgawanyo wa majimbo mapya yaliyotangazwa na Nec, lililokuwa jimbo la Mbozi Magharibi limegawanywa katika majimbo mawili ambayo ni Jimbo jipya la Tunduma na Jimbo la Momba.
Uamuzi wa kuachana na jimbo la Tunduma ambalo lilikuwa ngome yake kuu, Silinde aliutangaza juzi kwenye mkutano wa hadhara mjini Tunduma ulioandaliwa kwa ajili ya kumpokea baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge la 10 wiki iliyopita mjini Dodoma na kuhitimisha muda wa uongozi wa Silinde Mbozi Magharibi.
Silinde aliwaeleza wananchi kuwa sababu kubwa ya kwenda kugombea huko ni kutaka kuing’oa CCM.
RC K'NJARO AJITOSA
CCM Wilaya ya Songea Mjini mkoani Ruvuma, kimewataka makada wa chama hicho waliotangaza nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Songea kwenda kuchukua fomu.
Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Juma Mpeli jana aliwataja makada hao kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama; Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Arusha, Fransis Mitti; Katibu Mkuu wa CCM Wilaya ya Namtumbo, Azizi Mohamed Fakii, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia vyuo vikuu, Dk. Teresya Luoga; Mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Mussa Gama; Wakili wa Kujitegemea, Sebastian Waliyuba; Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea, Dornad Ndomba na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ufundi Mbeya, Erick Mapunda.
Alisema fomu zilianza kutolewa kuanzia jana hadi Julai 19, mwaka huu saa 10 jioni.
WANNE WAJITOSA ULANGA
Kwa upande wa mkoani Morogoro, wanachama wanne wamechukua fomu kuwania ubunge katika majimbo ya Ulanga Magharibi na Ulanga Mashariki kwa tiketi ya CCM.
Katibu wa CCM wa Mkoa huo, Rojas Romuli aliwataja waliochukua fomu za kuwania ubunge na majimbo kwenye mabano kuwa ni Issa Mfaume, Musa Maela Yasin Njayaga (Ulanga Magharibi) na Daudi Kindamba Kitowero (Ulanga Mashariki.
Kwa mujibiu wa Romuli, wagombea hao walichukua fomu hizo ambazo zilianza kutolewa jana na kuzirejesha.
Imeandikwa na Elizabeth Zaya Hussein Ndubikile, Hellen Mwango, Somoe Ng'itu na Theonest Bingora Dar: Said Hamdani, Lindi; Steven William, Muheza; Angelica Sullusi, Mbeya; Emmanuel Lengwa, Tunduma, Gideon Mwakanosya, Songea. na Christina Haule, Morogoro

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment