ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 26, 2015

NDEGE NDOGO YAANGUKA NA KUUA WATU WATATU NCHINI JAPAN

Watu watatu wamekufa baada ya ndege ndogo kuanguka nchini Japan, na kusababisha nyumba kadhaa kuungua moto.

Ndege hiyo ya viti vinne ilianguka baada ya kupaa ikitokea Chofu katika uwanja wa Tokyo, shirika la umma la NHK limeripoti.

Nyumba zipatazo mbili na magari mawili yaliungua moto, ambapo pia watu wawili waliokuwa kwenye ndege walikufa pamoja na mwanamke moja aliyekuwa kwenye nyumba.

No comments: