Wednesday, July 8, 2015

PROF. MWANDOSYA AWATAKA WABUNGE WA UKAWA WAINGIE BUNGENI KESHO



Waziri katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya ametaka wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhudhuria bungeni kesho ambapo rais ataingia bungeni kulihutubia na kulivunja bunge.



Prof. Mwandosya amesema jambo la rais kulihutubia bunge ni sula muhimu sana hivyo si vyema mbunge ama kundi fulani la wabunge kuwepo nje ya bunge wakati rais atakapokuwa analihutubia bunge.



Kauli hiyo ya Prof. Mwandosya ameitoa leo Bungeni, ikiwa siku chache tu kupita tangu Mkuu wa kambi ya Upinzani bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katika ya Wananchi (KAWA) Mhe. Freeman Mbowe kusema wabunge wa umoja huo hawatarejea tena bungeni.

2 comments:

Anonymous said...

Hii itashangaza sana kuona mh. Rais JK. Atakubali kulihutubu bunge lake la mwisho na kulivunja. Wakiwa hawa wabunge wa upinzani hawapo. Hakuna haki na sio utaratibu mzuri. Mheshimiwa spika anatakiwa alielewe na kuondoa kauli yake ya kuwakuza kwani nao ni viongozi wanaokubalika tuache manyanyaso kwa wawakilishi wa wananchi!! Rais lione hili usimwage vumbi zito kwa wananchi uloowaongoza muda wote.asante.

Anonymous said...

Nina kuunga mkono Anonym hapo juu. Hao wabunge waliopo nje ni wana siasa wazuri tu. Wapo nje sababu hawa taki kuburuzwa kisiasa. Tena wanaupeo wa kufichua maovu ya watendaji wa serikali bila kuogopa ama kuwalinda mafisadi. Kwa mfano halisi Mramba na Mkapa waliliti a hasara taifa Tsh 11 bilioni in a kuwa je a huku mi we hivyo? Amekutwa na makosa yote 11 lakini kapewa adhabu Sawa na ya kibaka. Lakini babu seya wa kuzushiwa Kahuku miwa maisha. UKAWA tumieni nguvu za wananchi please.....