ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 22, 2015

TAMASHA LA MZANZIBAR SALAMA BWAWANI ZANZIBAR

Mkufunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bibi Mafunda Nassor Juma akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi jinsi ya wanachuo hao wanavyojifunza upishi wa vyakula vya asili vya Zanzibar kwenye maonyesho ya uzinduzi wa Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibari hapo Bwawani Mjini Zanzibar.
Vazi lenye asili ya watu wa Kitumbatu walilokuwa wakilitumia wakati wakielekea mashambani huku mwana Mama anatembea akisuka ukili kuashiria ufundi wa utamaduni wa asili.
Vazi lenye asili ya watu wa Kitumbatu walilokuwa wakilitumia wakati wakielekea mashambani huku mwana Mama anatembea akisuka ukili kuashiria ufundi wa utamaduni wa asili.
Muimbaji mahiri wa Visiwa vya Comoro al anisa Shamsia Sagaf akitumbuiza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari hao Bwawani Mjini Zanzibar.
Msanii akionyesha msuko wa behedani uliokuwa ukitumiwa na akina mama wa enzi zile kwenye uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni.
Kikundi cha akina mama wakitumbuiza ngoma ya asili ya Lelemama kwenye uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AlI Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Waziri wa Habari,utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk pamoja na washabiki wa Tamasha wakimshangiria Kiongozi wa Ngoma ya Utamaduni ya Kiluwa akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanibari.
Baadhi ya wageni na watalii wakijipatia huduma za vyakula vya asili vya Mzanzibari kwenye uzinduzi wa Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya waswahili walioshiriki uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni wa Mzanzibari wakifuatilia matukio tafauti yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.

Waswahili waliovalia mavazi rasmi ya kiasili wakitafakari jambo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la Mzanzibari lililozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzi bar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.(Picha na OMPR)

No comments: