Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Moshi Shaban, kufutia kifo cha Moshi kilichotokea jana jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika leo jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Moshi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu Moshi Shaban ni baba wa wachezaji waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Haruna Moshi “Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).
TFF YAANDAA KOZI YA WAAMUZI WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2015/2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa kozi ya waamuzi wa mpira
wa miguu watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza 2015/2016, kozi hiyo itafanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 21 -24/08/2015.
Washiriki wa kozi hii ni waamuzi waliochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45 kwa wanawake na miaka 23 – 45 kwa wanaume.
Waamuzi wote wanatakiwa kuripoti tarehe 21/08/2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume Ilala Dar es salaam na wawasilishe vyeti halisi vya kuzaliwa na nakala zake.
Pamoja na cheti cha kuzaliwa kwa kila mwamuzi ni lazima alete kadi ya kupigia kura au passport ya kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa umri wake.
Washiriki wa kozi watafanya mitihani ya kupima afya, utimamu wa mwili na sheria za mpira wa miguu Trivia (kuandika), video clips (offside na match analysis).
Waamuzi watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi arobaini (40) na
waamuzi wasaidizi sabini (70) watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2015/2016. Shirikisho linawatakia wote maandalizi mema.
Baada ya kozi ya waamuzi kutakuwa na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ambayo itafanyika kuanzia tarehe 24/08/2015 hadi tarehe 25/08/2015.
Makamisaa wote wanatakiwa kuripoti tarehe 23/08/2015 saa 10:00 alasiri uwanja wa Taifa, Makamisaa watakao husika na kozi hii ni wale wote walio simamia michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2014/15.
Makamisaa watafanya mtihani wa sheria za mpira wa miguu (Trivia, offside, match analysis) na kupima mwamuzi anapochezesha (evaluation). Wale watakaofaulu ndiyo watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment