
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kutangazwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, katika uchaguzi uliofanyika Jana Julai 11, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM (Dodoma Convition Centre), uliopo Mjini Dodoma.
Dkt. Magufuli ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake, Balozi Amina Salun Ali akipata kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro akipata kura 59.





Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakipitia moja ya magazeti ya kila siku wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mjini Dodoma.
3 comments:
wenye akili,wenye kupenda amani na haki na kukomesha umasiki wa watanzani na haki sawa kwa wote katu hawatoipenda ccm na kuishangilia ILA KWA WAFUATAO UPEPO WASIO TUMIA AKILI ZAO, WANAOPENDA UFISADI,NA WACHUMIA TUMPO WATAIPENDA NA KUIPIGIA KURA CCM.
Eti leo wamejivua magamba? kwi kwi kwi.Tanzania ni nchi ya chama kimmoja kizazi cha leo hakidanganyiki;wameingia vyama vingi ili wawadanganye wafadhili na kupata misaada.
hawatupati ngo'oo ng'oo.watashinda kwa goli la mkono tu.
magufuli amefanya nini kuondoa umaskini wa watanzania ulio kithiri,amekemea lini ufisadi wa ccm je ana nguvu ghani au atakuwa na uwezo wa kupigana na mafisadi magamba wenzake ndani na nje ya chama?
je ana uwezo wakupigana na wauza unga ndani ya chama chake?
mwenye akili atang'amua.
hawatupati ng'oo kushinda watashinda lakini kwa BAO LA MKONOOOOOOOO.KAMA KAWAIDA YAO.
DJ BANIA COMMENT HII NI NGUMU KUIMEZAA.
sisiemu wametumia mbinu poa sana na kinana kishamwaga sumu vijijini watu waimbe tu sisiemu.nawaisome number.
mpenda maendeleo ya nchi yetu na mpinga ufisadi.ajiulize sufuria likipikiwa haramu halafu utoe hicho chakula cha haramu;na kuwapakulia watu je kuna watakao kula wanao juaa hicho chakula cha haramu?
unamfunga mtu kamba halafu unampiga;halafu unadai umemshinda;kwa nini usimuachiye apigane na wewe akiwa huru bila ya kufungwa kamba?uwanja wako,refa wako;mpiga wako usiposhinda si utaonekana mjinga sana.
Post a Comment