Wafanyakazi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani wakihakiki majina ya wageni waalikwa kwenye tafrija fupi ya Ubalozi huo ya kumuaga Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulumula (hayupo pichani) ambaye ndiye aliyekua Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani. Tafrija hiyo fupi ilifanyika Alhamisi Julai 23, 2015 kwenye jengo la Ubalozi lililopo mtaa wa 22, Washington, DC. Picha na Kwanza Production na Vijimambo.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi Donald Teitelbaum mmoja ya wageni waliofika katika tafrija na aliyekua msemaji mkuu Balozi Donald Teitelbaum ni Duputy Assistant Secretary for Afican Affairs.
Mshereheshaji Tuma akisherehesha kuagwa kwa Balozi Liberata Mulamula.
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka akisoma hotuba kwa niaba ya Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wakimtakia Balozi Liberata Mulamula Safari njema, kazi njema kule aendako, daima tutakukumbuka na kazi nzuri ulioifanya kwa muda mfupi uliokua nasi hapa Washington, DC daima itabaki kama kumbukumbu ya ufanyaji kazi wako ambao ni mfano wa kuigwa. Hayo yalikua sehemu ya maneno kwenye hotuba hiyo.
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka akimzawadia Balozi Liberata Mulamula zawadi kwa niaba ya Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma hotuba ya kumuaga balozi Liberata Mulamula kwa niaba ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York.
Balozi Donald Teitelbaum akisoma hotuba ya kumuaga Balozi Liberata Mulamula kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani huku akiwachekesha wageni waalikwa alipomalizia hotuba yake kwa kusema maneno ya kiswahili " Balozi Liberata Mulamula ni kiboko" akiwa anamaanisha ni mchapakazi.
Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake ya kuwaaga wageni waalikwa wakiwemo Mabolozi, marafiki wa Tanzania na taasisi mbalimbali zinazotangaza Tanzania nchini Marekani wakiwemo Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi na Jumuiya mbalimbali za Watanzania nchini Marekani
Wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Liberata Mulamula.
Picha ya pamona na Mabalozi na baadhi ya wageni waalikwa.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
1 comment:
such a great leader, so long mama balozi
Post a Comment