Advertisements

Saturday, July 4, 2015

WAZIRI KOMBANI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani akiwahutubia wajumbe waliohudhuria Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (Kulia) akipiga makofi mara baada ya Mgeni rasmi kufungua Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu wa Baraza hilo Magreth Jacob.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa mwaka 2014 Joshua Mwaisemba mara baada ya kufungua Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani akimkabidhi hundi mmoja wa wastaafu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ibrahimu Masanja mara baada ya kufungua Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua Kikao cha Pili cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Dodoma.

No comments: