Advertisements

Tuesday, August 4, 2015

BARAZA KUU LA CHADEMA LARIDHIA DKT SLAA KUPUMZIKA.


Hatimaye baraza kuu la Chadema limeridhia kusimama kwa muda kufanya kazi za chama aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod Slaa.
Ni kishindo cha baraka za baraza kuu la Chadema likiridhia kupumzika kwa Dk Wilibroad Slaa ambaye tangu kujiunga kwa wazir mkuu mstaafu Edward Lowassa amekuwa haonekani katika vikao vyetu vya chama hicho, katika ufunguzi wa mkutano wa baraza kuu la Chadema mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe amekiri kuwa licha ya Dkt Slaa kushiriki vikao mbalimbali vya chama kuhusu ujio wa lowassa, lakini ni kweli alitofautian kimtizamo na wajumbe wa kamati kuu. 
Aidha Freeman Mbowe amekiri pia juu ya hofu iliyokwisha kutanda kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ujio wa baadhi ya vigogo kutoka ndani ya chama cha mapinduzi CCM.
Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa Chadema taifa Salum Mwalimu akizungumza katika mkutano huo pamoja na masuala mengine amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuahkikisha wanaunganisha nguvu hasa katika kipindi cha uchaguzi.
Miongoni mwa agenda kuu zilizojadiliwa katika baraza kuu la Chadema ni pamoja na agenda ya kupitisha ilani ya chama hicho, kupendekeza majina ya wagombea nafasi ya urais ikiwa ni pamoja na kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu.

8 comments:

Anonymous said...

Hakika viongozi wa Chadema mnaumwa vichwa, yaani tuwaite VICHAA! Mnamtoaje shujaa ambaye alipiga jembe na kuchapa kazi kubwa na nzuri sana kukijenga chama chenu na mkamuingiza FISADI ambaye alikuwa ameshakataliwa na CCM? Uongozi wote wa Chadema needs MENTAL EVALUATION,seriously! This is laughable and pathetic. Is this a trade-off? You are kicking out the best mind, and Chadema's ROCK STAR and substitute him with a CCM reject? Shame on you Mbowe and your gang of MAFISADI at Chadema. Sadly, Chadema/Ukawa is doomed. Dr. Slaa has millions of followers, who will exit Chadema with him. This is another Lowasa's engineered scandal; unfortunately, this time around his tactical mission is TO SLAUGHTER the opposition in Tanzania. Pity to you, the Chadema/Ukawa leaders who pocketed the millions of shillings in bribe from Lowasa (Escrow style!). We never knew that Chadema/Ukawa was on the auction block to the highest BIDDER (Lowasa). Apparently, you have crushed the dreams of many poor Chadema followers, who will never again realize the much lauded Ukawa theme song "SAFARI YA MATUMAINI" come to fruition! Say What? SAFARI to where?

Anonymous said...

Ndugu yangu Dr Slaa naomba nikupe somo moja kubwa sana ambalo pamoja na udaktari wako ulio nao hili hukulifahamu. ASILIMIA KUBWA YA SIASA NI UNAFIKI MTUPU. ndio maana mashehe na makasisi hawafai kuingia kwenye siasa. sasa daktari wangu nakuamini wewe ni mtu muadilifu hivyo umeshindwa kuuvumilia huu unafiki wa wazi wazi unaotokea wakati huu ndani ya chama ulichokitumikia kwa moyo wote na nguvu zote. Ona wenzio wakina Mbowe waliobobea unafiki wako tayari kunywa mkojo na kula mavi na matapishi kama walivyo wachawi lakini wafanikishe lengo. Nakupa high five pumzika kwa salama siasa huiwezi wapishe wenyewe, soma alama za nyakati kwa heri.

Anonymous said...

Tusidanganyane hapa Dr. amesusa kwa ajili ya taama zake za madaraka ya kuwa rais kwa ndoto, pia na mkewe anachangia kwa kiasi kikubwa kuleta utoto huu. Huyu jamaa hataweza kuishinda CCM hata kwa dawa ni upotezaji wa muda na uelekeo , na nyinyi wote unaoleta biashara za mbowe kuongwa na fisadi hamjui mageuzi hata siku moja. Lowasa ana serikali nzima na hata watu wa usalama wa taifa, jeshi na waCCM chungu mzima wanamuunga mkono.Hata CCM wangejua jamaa EL anakimbilia upinzani wangefanya maamuzi mengine kabisa. wabongo hawaamini kama CCM inaweza kung'oka lakini iking'o ndiyo watajua kwanini CDM walimpokea ENL. Hata Obama alipokuwa anataka kuwa rais wa marekani hata weusi wenzake hawamunga mkono walikuwa wanajua haiwezekani badaya ya kushinda jimbo la Iowa (lenye wazungu) kwenye kura za maoni ndiyo weusi wakafunguka na kusema "Yes he can" hivyo msipotozwe na mpumbavu mmoja anayefuata mawazo ya mkewe, badala ya kuunga mkono EL ili we hata waziri ama agombee jimbo ili awe PM analeta utoto wa kuifanya CCM ishinde uchaguzi.

Anonymous said...

This is the most ridiculous and weakest argument ever put forward in modern history!

It's only in Africa, in general, and in Tanzania, in particular, where a grand corruption perpetrator is revered as a hero or liberator. Who on earth makes a hyena in charge of looking after his or her goats or a wolf in charge of looking after his or her sheep? Clearly, it's not an accident that Africa is the least developed continent on earth.

CDM and UKAWA, you have sold us down the river and I cannot wait to revenge come October 25!

Anonymous said...

Wewe anon. 4:49 AM, ni kwanza ni fisadi papa uliyelambishwa pesa za kifisadi na Edward Lowassa kama walivyolambishwa viongozi CHADEMA na UKAWA.

Kwa ufahamu wangu mdogo sana nilionao wa elimu ya darasa la saba, Lowassa hana uwezo wowote wa kushindana na Magufuli. Kumbukumbu zinadhihirisha kwa umma kuwa Magufuli ni mchapa kazi mzuri na muadilifu, tofauti kabisa na fisadi papa Lowassa. Hata unaposema ana Serikali yote, Usalama wa Taifa na Jeshi, unadanganya waziwazi hata mtoto mdogo anafahamu kuwa vyote ulivyovitaja viko kwa nani.

Siku UKAWA wakimtangaza Lowassa kuwa mgombea pekee, kabla ya kuanza kampeni CCM wanaweza wakamfungulia mashitaka ya RICHMOND, na akawafuata mafisadi papa wenzie akina Mramba na Yona kwenye safari ya matumaini, kabla hata ya uchaguzi wa Oktoba. Nao walikuwa wakisema kama wewe wana Serikali na Jeshi. kumbuka kesi huwa hazifi, kisheria. CCM wanaushahidi wote wa kumtupa jela Lowassa kabla ya Oktoba na ikawa mwisho wa safari ya matumaini.

Dr. Slaa ni jembe pia kama Magufuli, ndio maana kakataa kulambishwa hizo pesa za kivisadi kama walivyolamba viongozi wa CHADEMA na UKAWA. Wakakubali kula matapishi yao, akina Mbowe na Tundu Lissu, kweli nimeamini bongo hakuna upinzani.

Pia usimfananishe Lowassa na Obama hata kidogo. Obama wakati akigombea hakuwa na kashfa kama alizonazo Lowassa, tena Obama si mtu tajiri. Utajiri wa Lowassa ni wizi wa mali ya umma. Wakati akianza kazi baada ya kumaliza shule, alikuwa ni mtu maskini sana, na katengeneza utajiri mkubwa kutokana na nafasi alizozishika. Kwa haraka haraka pesa zake zote alizoiba Serikalini ziko mikononi mwa Rostam Aziz, Karamagi na vijisenti ( Chenge).

Wewe na wenzako wote mafisadi papa mwisho wenu umefika, raisi wa Tanzania mpya ya waadilifu na wachapa kazi atakuwa ni Magufuli na atateua mawaziri waadilifu na wachapa kazi akina Mwakyembe, ili kwa mara ya kwanza nchi irejeshe heshima yake.

Lowassa anakwenda kuwamaliza mafisadi wenzake aliowanunua akina Mbowe, Lissu, Lipumba, Mbatia, Makaidi na wenzao. Wao wamejipanga kwa kutumia pesa nyingi walizoiba kuwanunua wananchi ili waweke mtu wao na kuendeleza utaratibu wa wizi waliouzoea kwa kuwa wanafahamu fika kabisa, kwa Magufuli hakuna fisadi atakayesogea. Na sisi watz tumefahamu hayo na tunakwenda kuwaaibisha UKAWA na njaa zenu mwezi Oktoba.

Namuunga mkona Dk. Slaa kwa asilimia mia moja na moja, matokeo yake tutayaona mwezi Oktoba. Itakuwa kama yaliyompata Mrema miaka ile. Sisi wobongo hatuwezi kuwakabidhi nchi mafisadi na watu wenye njaa kama UKAWA.

Anonymous said...

Kwa kweli nampongeza dk slaa kwa nsimamo wake sasa naanza kumwamini kuwa ni mkirsto wa kweli sio lowasa anaejisifia kuwa yeye ni mkirsto wa kweli wakati huo huo anasema anawachukia watu masikini mkirsto wa aina gani kama si ufisadi mtupu? Kama Jesus angelikuwa karibu na lowasa wakati anajinasibu kuwa yeye ni mkirsto wa kweli tayari alishamdhaba kibao licha ya kuwa yesu kitu hicho ni vigumu kwake kutenda. Dk slaakutokufanya kazi na fisadi kwa kweli ametuthibitishia kuwa yeye si mnafiki na mtumishi wa Mungu as kweli..

Anonymous said...

tamaa mbaya sana Mbowe na mkwe wake walitaka yeye awe rais, lakini pingamizi ilikuwa Slaa kwa kuwa alishajijenga na umma ulijua ndie atapewa tiketi ya ukawa kwa uadilifu wake, yaliotokea yametokea hadi Lowasa kuitwa mkombozi ni kinyaa,atakapokuwa rais wanaomzunguka ndio wataofaidi na biashara zao,mbowe who?

Anonymous said...

Uchaguzi Oktoba ni CCM-A na CCM-B. Hakuna cha Chadema wala CuF!!! Wanasiasa Bwana kutafuta pesa popote pale!!! Maskini Slaa. Kashindwa kumeza matapishi yake!!!