ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 11, 2015

Dr. Slaa ameibuka tena kupitia Ukurasa wake wa Twitter na kusema mambo mazito kuhusu Lowassa.

Jitiririshe hapa chini alichotwitter Dr Slaa juu ya yote yanayoendelea Ukawa.

13 comments:

Anonymous said...

KWA TAMAA YAKO YA MADARAKA UNALIALIA OVYO. HAUNA MVUTO WEWE SLAA NA WALA HUFAI, HAKUNA MWENYE SHIDA NA MAISHA YAKO. WEWE KAA PEMBENI HAUNA LOLOTE UNAONGEA UJINGA TU WEWE SLAA....WEWE SI ULITOKA CCM PIA, UNA TOFAUTI GANI NA LOWASSA ALIYETOKA CCM???? WEWE UNA SKENDO ZA KUTOSHA UMEACHA UPADRI, UMEOA...UMEACHA MKE NA KUOA MWANAMKE MWINGINE HIVYO HUNA UADILIFU WALA UAMINIFU. ULIKUWA UNALIPWA KIASI KIKU.BWA CHA MILLIONI 11 NA HUKUTAKA KUKATA MSHAHARA WAKO. UNA TAMAA

Anonymous said...

Dear blogger, inabidi uwe unafabya kazi zako kwa makini ikizingatia wewe uko nchi za mbele, sasa umeshindwa hata kujua hiyo ni account fake ya Dr slaa, jamaa haitwi WILLIBRORD bali ni WILBROD (thats number one), pili ningetemea wewe bloger ambao kuna watu wankuamini sana Habari zako ungekuwa unafanya uchunguzi wa habari zako kabla ya kuzipaisha hewani na pia ungekuwa unamfollow Dr slaa na viongozi wengine kwenye twitter yake ili uwe unapata update zenye uhakiki, sasa inaonekana hata twitter account hauna aua haufuatilii kuchunguza habari za mtaani kabla ya ku publish..ushauri wangu try to get news from trusted sources and do some homework!

Anonymous said...

Huyu nae vipiii Si ULIPEWA CHANCE YA KUGOMBEA URAIS UKASHINDWA SASA KINAKUHUMA NINI.??. ULITAKA UPEWE MARA YA PILI UNADHANI UNGEMTOA CCM, UNGETUCHELEWESHA TUNAOTAKA CHANGE BWANA INGETU COST ANOTHER 10 yrs. EMBU MWACHE LOWASA AWATOE CCM BWANA WE VIPI?

Anonymous said...

Pasua baba tema nyongo lako watanzania tupo mashahidi jinsi ulivyoijenga chadema na kuwa chama pizani madhubuti leo malahi wachache wamekiteka chama na kazi yote ulioifanya inaokena bure. Kwa kuwadhibu tunakuomba kampe nguvu zito kabwe na misaada tutatoa kukuwezesha.

Anonymous said...

Dr. Slaajina lake siyo Willibroad, mtu Fulani anajifanya Dr. Slaa. Hiyo Twitter acct ni fake. Punguza ushabiki kidogo tunafahamu nyie ni CCM. I hope comment yangu utaiweka kama ukipenda.

Anonymous said...

alishasema hiyo siyo account yake...

Anonymous said...

Hiyo account itakuwa fake.Tazama jina lilotumika hapo ni Dr Willbrord badala ya Dr Wilbrod.

Anonymous said...

HAHA!!HAHAH!!hiyo account siyo ya mzee slaa kwa taarifu yenu,CCM inabidi muhangaike jinsi kutatua matizo yenu,dua la kuku hilo....,lazima make safari hii.

Anonymous said...

Hakuna mtu mpuuzi kama huyo jamaa hapo juu, anayependa kuandika kwa herufi kubwa kila wakati. Mabandiko yake yote utayajua tu na yote yanafanana kwa kukosa substance. Sijui anadhani kubwabwaja kwake ovyo ovyo kwenye mitatandao ndiko kutamfanya Lowasa kushinda uchaguzi. Utaandika sana ujinga wako, lakini huo ujinga hautabadilisha utashi wa wapiga kura. Umelelewa kwenye familia gani wewe mwenzetu?

Anonymous said...

Nyie mnaoshabikia Lowasa kugombea urais nawas hangaa sana, hivi hamjishtukii kwamba mmeonyesha udhaifu mkubwa sana, kwamba kumbe mtu anaeweza kuongoza nchi ya Tanzania kupitia vyama pinzani hawezi kutoka ndani ya vyama hivyo, maana yake wooote wameoza, Bali viongozi mahari wako CCM.
Bila hata aibu mnamsimamisha Lowasa kuwa mgombea wa urais, mtu ambae mlimtuhumu kwa nguvu zenu zote mkitutangazia kuwa ni fisadi mkubwa na ushahidi wa barua za ufisadi wake mlisema mnazo, leo hii mtamwambia nini mtu mwenye akili na hekima zake ambae pia aliyaamini hayo ambayo mliyatangaza kwenye majukwaa, viongozi wenu wamedhihirisha kuwa hakuna hata jambo moja la ukweli wanalolisema, wooote wamejaa ubinafsi, kupenda sifa na uroho wa madaraka, kitu ambacho kinawafanya waseme lolote bila kujali kuna kesho na kesho kutwa.
Haya sasa badilisheni statement Lowasa aonekane safi kama kuna mwenye akili timamu atawaelewa,. Na Lowasa nae ameonyesha uroho mkubwa wa madaraka, anaona ni lazima awe rais hata kama atatokea pande ambayo hakuifikilia kuwa siku moja angekuwa huko, swali ninalojiuliza ni je, amejiandaaje baada ya uchaguzi atakapokuwa ameshindwa vibaya? Kitu ambacho ndicho hakika kitatokea, maana mtu yeyote aliyeko ukawa na nimfuatiliaji na mwamini wa yale yasemwayo na viongozi wa ukawa hatapiga kura ya ndio Lowasa.
Kwa sababu hiyo basi Lowasa ajiandae kupotea kisiasa kama mwenzake Mrema.
Big up Dr Slaa maana umeona mbali jinsi ambavyo watanzania wasingekuelewa kama na wewe ungekubaliana na upuuzi huu unaoendelea.

Anonymous said...

Mimi na washangaa hawa wanajifanya watu wa pinzani hasa chadema kila kitu cha kweli kinachozunguzwa juu ya manyago yanayoendelea katika chama chao wapo wakali na wabishi kuukubali ukweli jamani huo ni upuuzi . Ikiwa hii Twitter account ya hapo juu ni halisi ya Dr Slaa au ni fake ujumbe uliobeba ndani yake ni maoni halisi ya Dr slaa . Kwani yanatofauti gani na maoni ya mkewe aliyoyatoa hivi karibuni? Kwani kunatofauti gani kati ya kristofa na Christopher ? Hiyo account ni ya slaa na kifo cha lowasa na ukawa kisiasa kipo mikononi mwa Dr Slaa na lipumba hao ni viongozi waliyo kataa kununuliwa na lowasa au naweza kusema hawakuridhishwa na mgao wa hela chafu za lowasa. Wakaamua kutoka nduki. Nyinyi watu wa upinzani ni watu cheap mmetawalia na mawazo ya kutawaliwa kuliko kujitawala mnasubiri mtu aje kukufanyieni maisha wakati mnajua hao viongozi wenu wa upinzani wote ni wa utapeli mtupu. Kama mmeweza kununuliwa na lowasa vipi matapeli ya kihindi? Ambao wanamuombea magufuli mabaaya wakijua wamekwisha ikiwa takuwa raisi . Nani asiejua kuwa matapeli ya kihindi ndio yanayomdhamini lowasa? Nyinyi kazi kukaa vijiweni kuilaumu serikali ya CCM wewe mwenyewe umejifanyia nini katika maisha yako? Pengine hata huyo mkeo au mama yako wa kukuzaa unashindwa kumuhudumia unahangaika kwa kupoteza muda na rasimali juu ya ukahaba. Tangu lini waafrica hasa watanzania tukawa na akili ya kuvithamini vya kwetu? Yuko wapi Gadafi yote alowafanyia watu wake bado walimuona adui. Wakaona wambadilishe wamlete anaefaa. Iko wapi libya sasa? Kuna mtu aliefikiria ipo siku walibya watakuwa miongoni mwa wakimbizi wakubwa duniani? Sio kama hatuhitaji upinzani isipokuwa tunataka watu waje na hoja za msingi. Sio leo ccm na lowasa fisadi kesho yake anafukuzwa na ccm kwa ufisadi saa pamoja baadae upizani wanamkumbatia na kumuona shujaa ebo. Nyinyi watu wa upizani mpo timamu kiakili kweli?

Anonymous said...

Na mtaandika articles ndeefu !!ikiwezekana mfungue gazeti kabisa,mlikuwa wapi kuandika articles hizo alipokuwa CCM?wanaume wazima Kazi kutunga stori za mitaani,safari UKAWA wamezuia mpaka choo sijui mtajisaidia wapi.Mmejaribu kwa lipumba watu bado wamo tena utitiri,lazima yawashuke.

Anonymous said...

Wewe anon wa 11:13 PM nina wasiwasi na jinsi kichwa chako kinavyofanya kazi. Ninashangaa kwa nini Dj Luke ameweka huo upuuzi wako hapo. Umepewa nafasi ya kutoa maoni yako siyo nafasi ya kujibu maoni ya wengine...haupo kwenye debate ya shule ya msingi. Kama unaona huna cha kuandika funga domo lako chafu. Hapa tunaandika wastaarabu siyo watu waliolelewa vibaya kwenye familia zao kama wewe.