ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 9, 2015

Heshimuni Wanawake enyi Mbuluraz!

Hapa duniani naweza sema 99% tumezaliwa kwa mfumo mmoja tuu (1% nimeacha kwa wale wanao pandikiza mimba kutumia utaalamu wa kisasa). Lakini kwa 100% bila shaka yoyote nasema kuwa wote tumekuja hapa dunia kwa kutumia mwili wa mwanamke! Hivyo kama ni mtu mwenye akili timamu unaweza ona ni jinsi gani mwanake anaumuhimu sana katika dunia hii! Yani hata kama technology itakuwa advanced kiasi gani katika maswala ya uzazi lakini bado mwanamke atahitajika tuu!! Na ndio maana inchi zinazo litambua hilo wanaweka sheria kali za kumlinda na kuheshimu mwanamke.
 
Kwanini nimesema haya; nikutokana na kile nilicho kiona baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema kujitoa katika madalaka yake na watu haswa haswa wananachama wa Chadema walivyo amua kumtusi na kumshtumu mke wa Dr. Slaa. “Lakini huyu mzee Slaa ni mzigo kwakweli, mzee mzima kama huyu kushikwa akili na mwanamke ni aibu sana, hivi kweli huyu urais angeuweza kweli, kiongozi wa chama mkubwa unalipwa zaidi ya 7 per monthly bado posho na marupu rupu kibao lakini week sasa inaisha umefungiwa ndani na janamke kazini huendi? Hivi kweli unadiriki kumpa mwanamke password za social networks, aiseee huyu mzee mi nimemshusha sana thamani,” hiyo ni moja tuu ya baadhi ya maoni mengi ambayo yametolewa na watu juu ya huyu mama. Mengine siwezi hata andika humu kwasababu ya ukali wa lugha walizo tumia.

Ngoja nianze kwa kusema kwanza yeye mwenyewe amekanusha hizo shtuma na kusema ni uwongo na uwonevu! Sasa nyie mbuluraz mliomtukana mlitumia kigezo kipi? Au kama kwaida yenu sikuzote mnamtupia lawama mwanamke? Si ndio tatizo la mfumo dume wa Tanzania ambao wanawake wa Tanzinia na wengine duniani wanaupiga vita?! Kumkandamiza mwanamke na kumuonea bila sababu tena katika karne hii 21 halafu mnasema manataka mtawale inchi? Ni inchi ipi hiyo? Inaama Chadema ikichukua inchi haitawasikiliza wanawake katika kufanya maamuzi magumu ya inchi? Are you guys serious?! Au ni inchi nyingine wezetu mnaongelea ambayo haina wanawake? SMH!

Halafu embu tuwe wakweli, mnasema eti Dr. Slaa hana maana kwasababu anamsikiliza mkewe?! Really? Nyie militaka amsikilize nani wakati huyo ndiye ambaye kila siku wako naye kwenye mabomu ya machozi? Mbona hata sikumoja hatujawahi kumuona mke wa Mwenyekiti wenu (Mrs. Freeman Mbowe) kava gwanda yupo jukwaani kwenye jua kali akinadi sera za Chadema kama kweli anapenda maendelo ya inchi hii ambayo mume wake anayapigania? Hatujawahi ona hata watoto wa Mbowe kwenye magwana wapo jukwaani halafu leo hii mnasema Dr. Slaa asimsikile mkewe? Inapanda akili hii kweli? Shame on you all! Kama mkeo hajawahi kupigwa kama mke wa Dr. Slaa kwa kutete chama chake basi nyamaza na mmuache Dr. na mkewe huyo huyo ambaye nyinyi mmemuona hakufaa kuwa first lady wenu yeye ndo kesha muona na anajua she’ll always be his first lady! Kama vipi kumywa vinegar changanya na tangawizi! Soma zaidi

8 comments:

Anonymous said...

Mbona unakurupuka kuandika usichokieleza kikakaa akilini mwa wapenda amani ama umeamua kuchochea moto wa petroli kwa nusu lita.!!?? Unazima baada ya dakika chache.! Na hautaunguza!!.

Anonymous said...

What is Mbuluraz. Mbona nawewe mwandishi unaleta matukano kwa watu wasiohitaji matatizzo? Je umeagizwa na Dr. Au Mkewe. Mbona ni watu wametulia hawataki vurugu Dr. Kajikalia kimya akifanya maombi hadi arejee ofisini kampeni zikianza tarehe 22. Wewebunaleta ichonganishi sio vizuri. Labda CCM wamekutuma. Tumekusoma.

Anonymous said...

Na wewe wacha uwongo wako na kuidanganya nafs yako pamoja na wenzako we are getting bored and tired listening this nonse. Dr Slaa and Chadema is over . Hiyo tarehe 22 unayosema atakuja kwa ajili ya kampeni ni kuweweseka mchana. Kwanini mnapenda kumdharau mtu wa mungu . Yeye alishasema kuwa lowasa ni fisadi hafai kuongoza taasisi ya uma yeyote nchini sasa kwa mantiki gani mnafikiri Dr Slaa atarejea kula matapishi yake?

Anonymous said...

mmh! mie naona hata nyie watowa maoni hapo juu mmekurupuka, au ni mtu mmoja.....mie naona mwandishi ana point embu soma vizuri mpaka mwisho

PETRO said...

Rubbish, hatuna

Anonymous said...

Msiguswe? Hiyo CCM itahonga wangapi? To wenu hoja

Anonymous said...

Hahah! And what' rubbish?

Anonymous said...

CCM
Siipendi mbona mnahangsika kuipaka Chadema
Dr slap na mkewe wapo Chadema na mtajuta atakapoibuka
Hatuangalli Magufuli wala Mafunguo
Kumbe unatuogopa UKAWA