Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati alipotembelea makao makuu ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam na kuzungumza na viongozi na wafanyakazi na kuwaaga rasmi leo Alhamisi Agosti 20, 2015.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Tom Nyanduga akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kuboresha haki za binadamu na Utawala Bora nchini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuhutubia na kuagana rasmi na wafanyakazi wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serkali Mh.George Masaju.
Rais akitoa hotuba yake ya kuaga
Rais akiteta jambo na mwenyekiti wa tume hiyo, Mh. Nyanduga
Rais akiagana na baadhi ya watumishi wa Tume hiyo
Rais akiagana na Mwenyekiti wa Tume, Mh. Nyanduga, kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Asha Rose Migiro. (Picha na Freddy Maro wa Ikulu)
1 comment:
Tunzo utawala bora
Kumfukuza kazi waziri kwa kashfa ya rushwa
Na kumpitisha ex waziri huyo huyo kugombea ubunge in utawala bora jamani
CCM mpo
Post a Comment