Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akikanusha jeshi hilo kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa. Kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.
"Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa.
Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.
Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo.
"Wananchi na viongozi wa kisiasa mnaombwa mfanye kazi zenu za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa wananchi" alisema Kanali Lubinga.
Kanali Lubinga alisema jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani wananchi wanaimani na jeshi lao.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

3 comments:
Mbona hili mnajibu haraka sana
Limewagusa na Lina ukweli
Meno ya tembo Zurich hadi Leo si serikali wala vyombo vya dola kutuelza ukweli
Au vigogo wa CCM wapo humo
Watu wa CCM. Wamvalia njuga Lowassa kila kona
Eti polisi nao wamekuwa CCM toba
Tatizo sio mgombea , tatizo ni sera za chama ndio watu wamezichoka. Hamna jipya ni longo longo tu utafikiri watu hawajui. CCC mwisho mwaka huu na mimi mazishi yao sitoi hela ya sanda. Magufuli anaweza kuwa yuko poa lakini hilo litabu ya ilani ya chama chake zinamtulisha kama maji ya kwenye mtungi. Akikohoa tu, wanamkolimba. Wanajua wenyewe Sera zao za kubanana pumzi.
Si wachina waliokaa kariakoo wakichoma mahindi. Tumevamiwa na watu hadi majumbani kwetu wananchoma mahindi, lakini hili hamjaliongelea> kisa? Lakini hili tuu la kuhakiki kadi za kura, mnalijibu haraka haraka, au kuna chembe chembe za ukweli? Tutajua tu si punde. Intellegencia ya watu wa nchi hii wanaotaka mabadiliko ni kubwa kuliko mtu mmoja mmoja au taasisi moja moja! Mungu atatuvusha tu salama, inshallah!
Post a Comment