ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 11, 2015

Lowassa achukua fomu za Urais Nec, maelfu wamsindikiza



EDWARD Lowassa, mgombea urais wa Chadema amesema, Rais Jakaya Kikwete ameharibu uchumi wa Tanzania.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho jana mchana, Lowassa alisema;“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”Aidha Lowassa alisema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” alisema Lowassa.

5 comments:

Anonymous said...

Usitudanganye Watanzania bwana Lowasa,na usikope campaign slogans za Western world. Kwa nini wewe umetajirika sana katika kipindi hiki cha Urais wa JK wakati mamilioni ya sisi wananchi tumezidi kuwa na umaskini? Kama uchumi ulikuwa mbaya sana kama unavyodai, wewe ulipata namna gani hayo mabilioni? Please, you are a practising Christian, hivyo ni dhambi kutosema ukweli. Ebu waambie ukweli Watanzania, badala ya kumlaumu JK. Besides, JK is a trained economist by profession, and thus, he knows better when it comes to economical matters.

Anicetus said...


Lowassa kasema: .."Rafiki yangu Jakaya kikwete ameuharibu uchumi wa nchi hii..." Kama kweli Lowasaa alikkuwa rafiki wa kweli wa President JK, kwanini hakuweza kumwambaia ukweli au kumuongoza kwa kitaalamu ili uchumi wa nchi undelee kuimarika. Where is the true friendship between Lowassa and the president.

In other words, Mr. Lowaassa accepts a friend when he is in need at any cost; he is prepared to prove their friendship by their deeds.

..A friend in need is a friend indeed..

Anonymous said...

1 USD = 2105.45 Tanzanian Shilling.
1 USD = 727.58 Rwandan Franc

Haya bishana na hizo Arithmetics hapo juu!!!..
Huyo JK kaharibu kabisa uchumi wa nchi!! Kila siku safari za nje tu!!
IMETOSHA IMETOSHA!! TUNATAKA MABADILIKO NJE YA CCM!!

Rwanda mwaka 1994 ilikuwa hata serikali haina kila kitu kilikuwa chali LEO hii hao wameshatupita. Waswahili kweli taabu tupu halafu hata ukweli hawataki kuusikia.

Anonymous said...

Exchange rates does not determine whether one country is better than the other. A Euro is stronger than a dollar, but none of the European countries are economically stronger than the U.S. Hivyo wewe mdau unayebwata kwamba Rwanda wapo mbele kuliko Bongo huna facts. Sijui Rwanda gani unayoizungumzia. Wametupita kwa lipi mdau? Tanzania is the second largest economy (nxt only to Kenya) in East Africa. Unazungumzia nchi ambayo bado iko kwenye political instability, ambayo inazo poor infrastructures, medical facilities, etc.. Acheni ushabiki usio na manufaa. I am proud to be a Tanzanian, and we are moving on, it took China centuries to become an economic power, second only to America! Tanzania's vision for 2025 is to be an economic giant in East Africa. People like you and your Ukawa/Chadema surrogates are beating drums of fear, to mislead wananchi. Nchi inasonga mbele bwana wee, pole pole ndo mwendo, na tutafika, na CCM pekee ndiyo inayo excellent long-term economic policies for the country, take it or not!

Anonymous said...

mchaka mchaka chinja unajua jamaa nampenda sana lakini kwanini ume mkopi makufuli hii slogan.na jambo la pili you are practicing Christianity unajaribu kuficha sana lakini watu tumeshajua njama zako.eti mkapa leo wakusifiwa wakati kaji binafsisha mgodi;mabiashara kibao leo kawa yeye wa maana.na jk kawa adui kisa kakukata; ndo kawa mbaya come on man I will vote for you but sema ukweli bwana lowassa.

hata mungu anapenda msema kweli.msema kweli mpenzi wa mungu.