Katibu Muenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa chama hicho utaofanyika kesho viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Picha zikichukuliwa.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza ratiba ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Katibu Muenezi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Juma 'Gadafi' akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo asubuhi, alisema maandalizi yote ya uzinduzi huo tayari yamekamilika.
"Maandalizi yote tayari yamekamilika na leo jukwaa kubwa la kukaa viongozi linafungwa na tunategemea kuwa na watu wengi katika uzinduzi huo" alisema Gadafi.
Gadafi alisema kuanzia saa tatu asubuhi watu kutoka sehemu mbalimbali na wapenzi wa chama hicho wataanza kuwasili katika viwanja hivyo ambapo viongozi wastaafu wa chama na serikali na wale waliopo kazini watafuatia na kisha watawasili mgombea nafasi ya urais kupitia CCM Dk.John Magufuli na mgombea mwenza wake Samia Hassan Suluhu na baadae Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Alisema katika uzinduzi huo wageni mbalimbali wamealikwa kutoka mikoa ya jirani na mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Gadafi alisema kuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo viongozi wa chama hicho wakiwemo mgombea urais Dk.Magufuli na mgombea mwenza wake watahutubia wanachama kuelezea sera za chama hicho na utekelezaji wa ilani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu.
Gadafi alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi, wanaccm na makundi mengine kufika katika uzinduzi huo ambapo kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya burudani na kufanyika kwa dua za madhehebu yote za kukiombea chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu kama inavyofanyika vipindi vyote wanapo zindua kampeni za uchaguzi mkuu.
Katika hatua nyingine Gadafi amekemea vikali vitendo vya udhalilishaji kwa wanachama wake vya kuzomewa na kuchaniwa nguzo zao wanapopita maeneo ya Kariakoo na Mwenge.
Alisema kila mwana chama yeyote wa chama cha siasa ana haki ya kuvaa nguo za chama chake hivyo kuwazomea wanachama wao ni kukiuka sheria ya nchi na inaweza kuleta ugomvi pale upande wa pili utakapoamua nao kujibu mapigo.
"Napenda kuiomba serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova kukomesha vitendo hivyo dhidi ya wanachama wetu na kama wanaona tunawakera wasubiri majibu yao baada ya uchaguzi kwani CCM itachukua ushindi mapema huku wakibaki wakishangaa" alisema Gadafi.
3 comments:
Asante CCM yetu ndio tunaanza malumbano?? Mwenyekiti wa Chama Chetu hiki ameshaona mbali na nini kitatokea hapo October. Ameshasema hataki kufuatwa huko nyumbani kwake anakoenda kufanya mifugo na kilimo. Kama ushauri atakuwa tayari kuchangia na hatahusika na chama au siasa. Atajishughulisha pia na ofisi yake aliyokwishaandaa. Ameshaona mbalinkuwa hii chama aliyoongoza na yale waliyofanya kinyume kule Dodoma hayana mwelekeo mzuri hii ni chali na anajitoa kiulaini. Mheshimiwa Mwandosya ukiwa myu safi ni bora usijiingize kwenye hizi kampeni
kwani zitakuharibia. Heshima yako uliyaona na ukayazungumza tuliyasikia hii chama inaharibiwa na sisi wenyewe. January wa Makamba aliingizwa tano bora ilikuwa zawadi ya Mh. JK kwa kuwa mwandishi wake lakini hakumzidi Mwandosya. Kazi tunayo wachama. Business as usual.!!
Mtakimbiwa hata mama na baba zenu kwa ulafi wa madaraka ccm
Mwaka huu wenu
Hata mkiiba tutarudusha vyote
Tumechoka tumechoka kuishi ugenini kwenye nchi yetu wenyewe
Heeee yebaaaaaa tutata ongea yoteeee ila all in all October 26 tuuuuuuu watu peopleeeeeeeee
Post a Comment