ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 28, 2015

Magufuli: Nikishinda sina deni la fadhila.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema hana deni la kulipa kwa mtu yeyote akichaguliwa kushika wadhifa huo kwa kuwa hakutoa rushwa wakati wa uteuzi ndani ya chama hicho.

Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati akijinadi yeye na wagombea udiwani na ubunge wa CCM mkoani hapa ili wachaguliwe katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Dk. Magufuli alikuwa akijinadi na wagombea hao kwa nyakati tofauti katika mji wa Mbalizi na wilayani Songwe eneo la Mkwajuni, Makongolosi wilaya ya Chunya.

Magufuli ambaye jana alikuwa katika siku ya nne ya kujinadi kwa wananchi na kuomba kura tangu kufunguliwa kwa pazia la kampeni mikoani, alisema tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM wa urais ndani ya chama hicho, hakutumia fedha bali alikwenda kimya kimya makao yao makuu kuchukua fomu na kuzirejesha.

Alisema kwa mantiki hiyo, hana cha kulipa kwa sababu hadaiwi na mtu yeyote.
Magufuli alisisitiza kuwa anachofahamu ni kwamba deni kubwa alilonalo ni kuwatumikia Watazania na kuwaletea maendeleo ili wazidi kuwa na maisha bora.

“Nilichukua fomu kimya kimya na kurudisha kimya kimya, natembea na barabara ili shida zenu ziwe shida zangu, ili nikiingia Ikulu nizishughulikie kwa haraka,” alisema.

Magufuli alisema anaamini kuwa kuteuliwa kwake na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro hicho kuna makusudi ya Mwenyezi Mungu ili afanye kazi.

“Sikutoa rushwa kwa kuwa ni dhambi na adui wa haki... niliacha mchakato huo wa kumpata rais ndani ya CCM ufanywe na Mungu,” alisema.

AOMBA POWER
Dk. Magufuli alisema wale wanaosalimia kwa kutumia salamu na kauli mbiu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Peoples Power, wampe ‘power’ aende Ikulu kuharakisha maendeleo ya watanzania.

“Nipeni wabunge na madiwani wa CCM nikafanye kazi, tutafanyakazi bila kinyongo, hatutawabagua, hapa ni kazi tu,” aliahidi.

Alisema maendeleo hayana chama, kabila wala rangi, hivyo amepanga kufanya kazi na makundi yote bila kubagua na kuomba kura kwa wananchi wote bila ya kujali vyama vyao vya siasa.

“Hakuna anayezaliwa kutoka tumboni mwa mama yake akiwa na kadi ya chama fulani, bali wanavikuta, hivyo msidangaywe na vyama, kinachotakiwa ni maendeleo,” alisema.

WALIMU VUMILIENI
Akizungumzia kuhusu madai ya walimu nchini, alisema kada hiyo siyo wito bali ni kazi, fedha na kuwafundisha wanafunzi kwenye shule walizopangiwa na serikali.

Alisema baada ya kuingia Ikulu, kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuwalipa madeni wanaoyoidai serikali.

Magufuli aliwataka walimu kuwa wavumilivu na kuwaomba kumchagua kwa kura nyingi katika uchaguzi huo.

“Sitawaangusha, nitamtanguliza Mungu na kila mmoja katika sala zake aniombee nisijeanza kwa kiburi, kujiona, kusahau ahadi, niwe mtumishi wa watu, nikapendwe kwa utumishi na siyo bora utumishi,” alisema.

AWATANGAZIA KIAMA MAJANGILI
Aidha, Magufuli alitangaza kiama dhidi ya majangili wanaoshirikiana na askari wanyamapori kupora rasilimali za meno ya tembo na pembe za ndovu huku akishangazwa na kitendo cha askari wanyapori kulipwa mishahara vizuri na wenye silaha kwa kushindwa kuwalinda tembo kwenye hifadhi za wanyamapori nchini na kuuawa na meno yao kukatwa na kusafirishwa nchi za nje.

Alionya kuwa serikali yake haitakubali vitendo hivyo viendelee.

WAKURUGENZI
Pia, Magufuli alisema serikali yake itapiga marufuku wakurugenzi wa halmashauri nchini kutembelea magari ya kifahari na kukaa kwenye majengo mazuri wakati wanafunzi wakisoma wakiwa wamekaa chini madarasani.

Alitangaza kuwa elimu itakuwa ikitolewa bure kwenye shule za serikali na kuboresha mazingira ya kusomea.

Magufuli alionya kuwa watakaoshindwa kwenda na kasi yake katika kutumikia wananchi, watakazimika kuachia madaraka.

MAADHIMISHO MARUFUKU
Kadhalika, alisema katika serikali yake itakuwa ni marufuku kufanyika maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa kuwa yana lengo la waandaji kulipana posho na kuvaa sare za fulana na kofia huku wananchi wakiteseka kwa kukosa maji safi na salama.

AWALIPUA WAPINZANI
Katika hatua nyingine, awalirushia kombora wapinzani, akiwataka wananchi wasiwachague kwa madai kuwa watasababishia mateso.

Alisema kwa sasa Tanzania inaelekea kwenye neema ya maliasili kama ya gesi, madini na wanyamapori, ndipo wapinzani wanajitokeza kuwalaghai watanzania kuwa wataleta mabadiliko makubwa.

AIAGIZA TANROADS
Katika hatua nyingine, Magufuli ameendelea kutumia wadhifa wake wa uwaziri wa Ujenzi kwa kumwagiza Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya, kujenga barabara ya kilomita moja mjini Mbalizi na kutangaza zabuni ya kilomita nne za barabara mjini Makongolosi ndani ya wiki moja.

Pia, amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Tanroads, kupeleka fedha za ujenzi na upanuzi wa barabara hizo ndani ya wiki moja.

Akihutubia mikutano ya hadhara mjini Mbalizi na Makongolisi, alimpandisha jukwani Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro na kumtaka ampelekee maagizo hayo Meneja wa Tanroads wa mkoa huo aliyemtaja kwa jina la Lyakurwa.

“Mimi bado ni Waziri wa barabara, ukifika ofisini mweleze Lyakurwa barabara hii ianze kujengwa, leo (jana) nampigia Chief Executive (Mtendaji Mkuu) wa Tanroads alete fedha haraka, wiki hii nataka kuona kazi inaanza...natamani ningekuwa rais nianze kazi leo niguse na sekta nyingine,” aliagiza.

Akiwa katika katika mji wa Makongolosi, alimuita jukwaani Kandoro na iagiza Tanroads kutangaza zabuni ya kilomita nne za barabara za mjini Makongolosi.

“Mimi napenda mambo yaende harakaharaka, uwaziri wa ujenzi bado ninao, tukitoka hapa RC mwambie Meneja wa Tanroads atangaze zabuni ya kilomita nne mjini Masongolosi zianze kujegwa na fedha nitatoa, nataka muone kuwa nasema na kutekeleza,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

8 comments:

Anonymous said...

Kuna watu respectable wenye CV zao za maana duniani…lakini walivyojihusisha na CCM wamechafua CV zao;
Mfano;
Getruda Mongela mwanamama aiyeongoza mkutano wa Beijing unajua kashfa za rushwa zilizokuja kumkumba
Sospeter Muhongo-A respectable Journalist unajua Amefanya nini kwenye ESCROW
Omar Nundu mtaalamu wa dunia wa usafiri wa anga unajua ni nini kimemtokea
Prof Anna Tibaijuka mama aliyeongoza shirika la Umoja wa mataifa unajua nini kimemtokea
Daudi Balali a respectable IMF and World Bank Economist unajua nini kimemtokea baada ya kujihusisha na CCM.
Ukiachana na hao…Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani alikuwa mtu mchapa kazi…Katika wizara alizopita kabla ya hapo alikuwa mwadilifu na Mchapa kazi…alichaguliwa kwa 80% kumbuka….Nini kimetokea baada ya kuwa Ikulu?
Benjamin Mkapa..Jembe la Nyerere aliingia kama mzee wa kazi ameondoka na kujimilikisha mgodi wa Kiwira.
Magufuli anayegombea urais wa CCM Alishiriki kikamilifu katika kuuza nyumba za serikali….Ameshiriki kuiingiza hasara serikali majuzi kwenye kivuko ca kigamboni shs Bilioni 8…Kivuko hakina muda wa miezi mitano lakini hakifanyi kazi ….ameiingiza hasara serikali kwa maamuzi mabovu mengi aliyofanya.
Ndio maana kwa tunaotazama mambo kwa umbali ni bora CCM ikakaa pembeni tuanze upya (Sio kwamba wapinzani ni wazuri sana)…Kutakuwa na maumivu ya miaka 5 lakini baada ya hapo tuta endelea kama taifa.
Kama taifa inabidi tuweze kufanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
Mfano kulikua na haja gani ya kumilikisha kampuni za wazungu gesi yetu kwa miaka 99…tena kwa mikataba ya siri…….
Utakuwa kichaa kudahani magufuli ataipitia hio mikataba na kuifumua…You must be mad

Anonymous said...

Kwa formula yake ,alie safi akiingia madarakani anachafuka, vipi umpe nchi aliyekwisha chafuka kwa kashfa za ufisadi? Hasa ukizingatia hata wakati akiwa CCM alikuwa already ni kinara wa rushwa na ubadhilifu wa mali za uma.
Si kila mtu ni mpumbafu na lofa (ref BW Mkapa) na asiejitambua..over

Anonymous said...

Wewe nawe acha kuongea pumba

Kwanza tangu lini Prof. Muhongo akawa Journalist?? Embu fanya research yako vizuri ndo uje hapa na mauza yako

Anonymous said...

How are you going to leave Lowassa in all those rubish accusation you spew above? Have you heard about Richmond scandal. Au ulikuwa umefungwa gerezani wakati huo or is just stupid amnesia coupled with seective memory. Come on brahh! Tell it like it is.

Anonymous said...

Mdau nimependa point yako naomba kupost Jamiiforum.

Anonymous said...

Mbona huongelee shs. 12 billioni alizopewa mkubwa wenu wa chama ili kumkaribisha huyo mwan-CCM ambaye muda wote mlimwita fisadi? Mbona huongelei mamilioni mkubwa wenu aloyowakatiwa akina Tundu Lisu na wenzake ili kuwanyamazisha na kuleta kasheshe ndani ya chama? Au ndio unatuambiwa kuwa hiyo ni sahihi. Natumaini umemsikia Mwakyembe alivyosema kwenye hotuba ....naachia hapo na mengine utaongezea.

Anonymous said...

MAGUFULI ACHA UONGO, UNA DENI LA FADHILA YA KIKWETE. PILI, WEWE UNATULETEA UONGO ULE ULE, WA AKINA CHE MKAPA NA KIKWETE. WENZAKO WALIOKUTANGULIA WALITUJIA NA TUME BUTU YA RUSHWA, TAKUKURU, HALAFU BILA AIBU HII TAKUKURU IMEBAKIA KUFUNGA MAHAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO NA WALIMU WAKUU, ILHALI MIJAMBAZI NA MIFISADI MIKUU IPO HURU. WEWE NAWE BILA AIBU UNATUAHIDI UPUUZI ULE ULE, MAHAKAMA YA UFISADI, AMBAYO KUTOKANA NA HISTORIA WALA SITASHANGAA UKIIANZISHA NA KAMA TAKUKURU, HII MAHAKAMA ITAENDELEA KUFUNGA WANYONGE, NA KULINDA MAFISADI PEMBE.

Anonymous said...

Mtu mzima hovyo . Mavi gani unayoyazungumzia kuhusu hizo CV? Msituletee uwongo mwepesi mwepesi hapa mkataka kuwadanganya watu huo upizani na hao viongozi wao hawafai kuongoza hata manispaa ya wilaya. Kwanza sio chama ni taasisi ya kikanda inayopigania maslahi binafsi kuliko utaifa. we kama usingekuwa mnafiki na fisadi wa mawazo katika hiyo ordha yako ya walioitumikia CCM na CV zao basi Eduwadi lowasa angelikuwa namba moja katika ubadhirifu . Mtu unaweza kujitoa fahamu usifikiri watu waliokaa pembeni na wao wametokwa na fahamu hilo msahau kabisa.