
NIJumanne tena, wapenzi wasomaji wangu tunakutana tena katika safu hii ya mapenzi na maisha. Ni safu inayokusudia kutoa elimu kwa wanandoa, wapenzi, wachumba na wengine wanaotarajia kuingia katika meli hiyo ya maisha ya mapenzi.
Mada ya leo inaweza kuwa ngumu kidogo kutokana na ukweli kwamba, inazungumzia misimamo ya taasisi za kutetea haki mbalimbali kujenga hoja ya kuwaambia wanaume wasiwe na mfumo dume.Lakini pia, mada hii itachota baadhi ya vipengele kutoka kwenye vitabu vya dini ili kuifanya kuwa na uhalisia zaidi kuliko mtazamo wa mwandishi.
KWANZA KABISA
Nianze kwa kusema kuwa, kumekuwa na hoja mbalimbali duniani kote kwamba, baadhi ya wanaume wanaishi maisha ya mapenzi kwa kutumia mfumo dume. Hivyo, taasisi zikaundwa, wanaharakati wakajitokeza kupinga matumizi ya mfumo dume kwa wanawake.
NINI MAANA YA MFUMO DUME?
Mfumo dume inasemwa kuwa ni ile hali ya mwanaume katika familia kuwa mwenye maamuzi pekee katika nyumba. Au kwa kifupi ni tabia ya mwanaume kuwa mtawala na mwenye kauli ya mwisho.
Wengine wanakwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, mfumo dume ni ile hali kwamba, mwanaume anaweza kuchelewa kurudi nyumbani lakini mwanamke akichelewa panachimbika kwamba alikuwa wapi? Au mwanamke akiomba ruhusa kwenda harusini, mumewe anaweza kumkataza kwa kumwambia ‘sitaki uende harusini’ lakini yeye akienda haombi ruhusa bali anatoa taarifa tu.
KWA UJUMLA
Kwa ujumla, mfumo dume unatajwa kuwa ni ile hali ya wanaume kuwa wenye maamuzi ya mwisho katika uhusiano, hasa familia. Mwanamke hatakiwi kutoa sauti mbele ya mwanaume kama yupo. Mwanaume akikosea hawezi kukosolewa kama akikosea mwanamke.
WAPINGAJI WA MFUMO DUME
Utafiti wangu ulibaini kuwa, watu wengi wanaopinga mfumo dume ni wanawake wenyewe. Wanajiita wanaharakati. Lakini pia kwa sehemu wapo wanaume ambao hawakubaliani na mfumo dume.
Kwenye nchi za Ulaya na Amerika, hasa ya Kaskazini wengi, wake kwa waume wamekuwa wakipinga mfumo dume. Sasa hivi wanaishi kwa usawa. Mwanaume anaweza kupika, mwanamke akasubiri kula. Mwanaume anaweza kufua nguo, mwanamke akazianua jioni.
NILICHOBAINI
Kikubwa ambacho nimekibaini ni kwamba, wanawake wanachofanya si kupinga mfumo dume. Bali wanatafuta uhuru. Kwamba, na wao wawe wanachelewa kurudi nyumbani, wasiulizwe. Wawe wanakaa baa mpaka saa tano, wasiulizwe. Waume zao, wawe wanawahi kufika nyumbani na kuandaa chakula kwa familia, wao wakiwa wamekwenda kwa marafiki zao, wasiulizwe. Ndiyo maana wimbi la familia kutaka wasichana wa kazi limekuwa kubwa kwa sababu ya kutaka nyumbani kuwepo mtu wa kufanya kazi za ndani wakati wanandoa wakiwa kwenye mihangaiko yao.
KINACHOPINGWA KIPO NYUMA YA MFUMO DUME
Nimekuwa nikizama kwenye vitabu vyenye maneno ya Mungu nikabaini kwamba, kinachopingwa na wanaharakati si mfumo dume. Ni matukio yaliyopo nyuma ya uwezo wa mwanaume katika kumtawala mwanamke tangu kuumbwa kwa dunia hii kama siyo ulimwengu.
Mwanaume akitumia nguvu zake kumpiga mkewe kwa sababu amekorofishwa si mfumo dume bali ni ukatili. Mwanaume akimbaka mtoto mdogo kwa sababu ya uwezo wake wa nguvu, si mfumo dume, ni ukatili na unyama.
Wapo wanaume, wanagombana na wake zao, kwa hasira wanawamwagia maji ya moto mpaka kuwaunguza vibaya sana. Huo si mfumo dume. Ni unyama uliopitiliza. Naupinga vikali.
Mada hii ni pana sana, itachukuwa karibu matoleo matatu.
Usikose kuisoma wiki ijayo kwa uchambuzi zaidi ili kuelewa lengo la mwandishi.
GPL
2 comments:
SIO KWELI KUWA "Kikubwa ambacho nimekibaini ni kwamba, wanawake wanachofanya si kupinga mfumo dume. Bali wanatafuta uhuru. Kwamba, na wao wawe wanachelewa kurudi nyumbani, wasiulizwe. Wawe wanakaa baa mpaka saa tano, wasiulizwe. Waume zao, wawe wanawahi kufika nyumbani na kuandaa chakula kwa familia, wao wakiwa wamekwenda kwa marafiki zao, wasiulizwe. Ndiyo maana wimbi la familia kutaka wasichana wa kazi limekuwa kubwa kwa sababu ya kutaka nyumbani kuwepo mtu wa kufanya kazi za ndani wakati wanandoa wakiwa kwenye mihangaiko yao." HUU NI UWONGO NA UPOTESHAJI. INAONYESHA!
Wanawake wanapigani kuondoa mfumo dume kwasababu wanataka kuona haki inatendeka katika maswala ya msingi kama:-
HAKI YA KUHESHIMIWA NA KUTHAMINIWA KAMA MWANAUME.
HAKI YA KUJUA NA KUTAMBUA MWANAMKE NAYE NI BINADAMU KAMA MLIVYO NYIE WANAUME, TUNAHISIA NA TUNA UTASHI KAMA NYINYI.
HAKI YA KUHESHIMU NA KUMSIKILIZA MAONI NA USHAURI WA MWANAMKE KAMA WANAVYO FANYIWA WANAUME. USHAURI WA MWANAMKE UPEWE UZITO KAMA ANAVYO PEWA MWANAUME.
HAKI YA KUTAMBUA KUWA HATA KAMA MIMI NI HOUSEWIFE BASI NAHITAJI KUSHIMIKA, KUTHAMINIWA KAMA MMOJA WA WATU WANAO CHANGIA MAENDELEO YA NYUMBANI NA INCHI KWA UJUMLA KWANI HATA KUKAA NYUMBANI KULEA WATOTO NA MAJUKUMU MENGINE YA NYUMBANI NI KAZI VILEVILE!
TUNATAKA HAKI YA KUTAMBUA KUWA MWANAMKE NAYE ANAUWEZO WA KUFANYA VYEMA KATIKA MASWALA YA UWONGOZI NA ELIMU HIVYO WAPEWE HAKI SAWA KAMA WANAVYO PEWA WANAUME!
HAKI YA KUTAMBUA KUWA MKEO SIO MWANAO HUNIPANGII SHERIA BALI TUNAJADILIA NINI CHA KUFANYA,
HUNIPIGI ETI KWASABABU NIMEKOSEA KWANI MIMI SI MWANAO KAMA NIKIKOSEA TUNAELEZANA KWA UPENDO
TUNATAKA MJUE KUWA MWANAMKE NAYE ANASAZI YA KUJAMIIANA AU KUTOKUJAMIIANA KWANI NAYE ANAHISIA KAMA MWANAUME....n.k
Sasa hayo uliogundua ni siyo yakweli labda ulifanyia research yako kwa wanawake wa baa tuu!!
umemaliza umesema yote niliyokuwa nataka kuyasema na mimi hapo juu mdau mwenzangu.kweli kabisa kafanya research ya wanawake wa baa lakini pole pole jameni una mhurt his/her feelings ha ha ha.
one thing tujiulize sisi wanawake kwa nini tuwe tunataka tupewe hizo haki why we cant take action tukisubiri ya kupewa hizo haki hatutopewa hatutozipata twende speed na hata mdogo mdogo na tuzichukue hizo haki.
mwanamme hatokaa kamwe akupe hizo haki unless he is a good and really a good man inside and outside other than that sahau kabisa kupewa hizo haki.
lets go and grab them ourselves.msome mume gani unaye/mkee ghani unaye na utajua vipi za kuzichukua hizo haki si ubabe hata kwa upole utazipata hizo haki but ikishindikana ubabe kidogo utumike.
nakupa heko mdau mwenzangu hako juu.hongera sana.
Post a Comment