ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 11, 2015

MKURUGENZI WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AWASHAURI VIJANA KUFANYA KAZI NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mada katika Kongamano la Vijana. Wakati wa kongamano hilo Balozi Mushy amewashauri vijana kufanya kazi na Taasisi za Umoja wa Mataifa ili kujipatia uzoefu wa kujielezea ikiwa ni pamoja na kujiamini. Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem (Wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Balozi Mushy (Hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mada.

Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.

Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana
Balozi Mushy (Katikati mwenye suti nyeusi) alipokuwa akiwasilisha mada ambapo pia alitaka kujua ni vijana wangapi wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2015, huku ikionekana idadi kubwa ya vijana waliohudhuria Kongamano hilo wamejiandikisha.

3 comments:

Anonymous said...

talk is cheap...

Anonymous said...

True, it is not easy to get hired by the UN agencies. Lots of corruption involved, on top of red-tapes and bureaucracies.

Anonymous said...

Viongozi wetu wanasema tuendelee kufundisha Kiswahili hadi chuo kikuu, sasa hapo utapata wapi kazi kwenye UN wakati huko wanahitaji advanced English? Huko UN wamejaa watu kutoka Senegal kwa sababu ya Bilingual, Wakenya/Waganda/wanyarwanda kwa sababu ya advanced English yao na uchacharikaji wao. Sisi tunabaki na hizi semina za cheap talks. Suala la kutafuta na kufanya kazi UN wala halihitaji semina na mikutano ni suala la kuchacharika.