VISA vimeanza! Siku chache baada ya nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupata ‘baby girl’ aliyempa jina la Latifah kupitia kwa mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari’ kuna madai kwamba, jina la Latifah limezua mambo, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya wanafamilia wa Diamond hawakubaliani na jina hilo wakitaka kichanga huyo aitwe Sanura, jina la mama Diamond wakiamini kuwa, ndiyo historia ya enzi na enzi, kwamba mtoto wa kwanza hurithi jina la mzazi wa baba ili pia ‘kukopi’ tabia. Latifah ni mtoto wa kwanza kwa Diamond.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Jamani mmesikia huko! Baadhi ya ndugu wa Diamond, wameanza kusemea chinichini, hawakubaliani na mtoto wa Diamond kuitwa Latifah. Wao wanataka aitwe Sanura, jina la bibi yake (mama Diamond). Wanaamini akirithi jina hilo atarithi hata tabia kwani mama Diamond ni mkarimu, mpole na mnyenyekevu kwa watu, lakini msimamo wa Diamond ni uleule, anataka mtoto wake aitwe Latifah,” kilisema chanzo hicho.
WENGINE WAGOMA…
Wakati baadhi ya wanafamilia wakitaka hivyo, wengine wasiofika idadi ya ‘wengi wape’ wamemuunga mkono Diamond kwa kumwita mtoto huyo Latifah.
“Lakini ndugu wengine wamesema Diamond hajakosea, mtoto aitwe Latifah kwa sababu hakuna tatizo wala si dhambi mtoto kuitwa kwa jina lingine mbali na la kurithi kwa bibi au babu kama ilivyokuwa zamani.
ZARI ASHANGAZWA
“Hata Zari naye ameshangazwa na mvutano huo wa jina kwani yeye anaamini mtoto anapewa jina lolote tu kulingana na wazazi watakavyoamua,” kilisema chanzo.
MADAI YA MSINGI
Habari zaidi zinasema kuwa, wanafamilia wanaotetea jina la mama Diamond, wamekuwa wakihoji lilikotokea jina la Latifah ambapo wanadai haliko kwa akina Zari wala kwao Diamond.
“Wao wanasema kama jina la Sanura waliliona halina mvuto, basi Diamond angemwita mtoto wake Sandra ambalo pia ni jina la mama Diamond.
“Unajua ndugu siku zote hawakosi la kuongea kukiwa na jambo hasa kama hili la mtoto maana mengi yataibuka lakini wazazi ndiyo wenye uamuzi wa mwisho,” kilisema chanzo.
KUMBE KUNA MAMA ZARI NAYE
Chanzo kiliendelea kuweka bayana kwamba, mbali na baadhi ya wanafamilia kutaka mtoto huyo kuitwa kwa jina la Sanura lakini pia kuna madai kwamba, mama wa Zari, Halima Hassan alipenda mtoto huyo aitwe kwa jina lake hilo kwa vile ndiye mjukuu pekee wa kike wa bintiye. Watoto wengine wa Zari ni Pinto, Didy na Quincy.
MAJINA YA KURITHI YANAVYOKUFA
Kutokana na utandawazi uliopo, watoto wanaozaliwa miaka ya karibuni hawapewi majina ya kurithi kama zamani kwa madai kuwa hilo lilishapitwa na wakati na kama mtu atarithishwa jina basi huenda akarithi na tabia na ni heri akute anayemrithi ana tabia njema.
“Unajua majina haya ya kurithi sijui kutoka kwa bibi au babu huwa yanazua balaa kwa maana wengi wanasema mtu akirithi jina basi huchukua hata tabia kitu ambacho inawezekana Diamond na Zari hawajapenda binti yao arithi jina kutoka kwa mtu yeyote,” kilieleza chanzo kingine.
JINA LA LATIFAH
Jina la Latifah a.k.a Princess Tiffah lilipatikana siku chache kabla ya kuzaliwa baada Diamond mwenyewe kuomba kwa wafuasi wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram wamsaidie jina ambalo litakuwa linatokana na imani ya Dini ya Kiislam.
DIAMOND APIGWA DONGO
Wakati jina la Latifah likizua hayo, rafiki wa karibu wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga, Kinglawrence amemtupia dongo Diamond akisema hakuhitajiki kipimo chochote cha vinasaba DNA ili kujua kuwa, Latifah si mtoto wa Diamond kwani mambo yamejionesha yenyewe baada ya miezi tisa.
Kwenye mtandao wa Instagram, jamaa huyo aliweka picha ya Ivan aliyoiunganisha na picha ya Latifah ili wadau waone walivyofanana. Hapa ana maana kuwa, mtoto huyo ni wa Ivan.
DIAMOND SASA
Diamond alipotafutwa aseme neno kuhusiana na madai hayo yote, alipuuza kuhusu mtoto ni wake au si wake, akasema ana furaha iliyopitiliza ya kupata mtoto na kuhusu jina haoni kama kuna tatizo.
GPL
2 comments:
Tutoleeni hizi habari za kizembe hamna cha maana cha kuposti
Inaweza kuwa mtoto si wake ila yeye ameridhika na kumtuza kama mtoto wake. hii ni uchuguzi wa Prez Diamond. kuna watu wengi sana wanatunza watoto ambao sio wao yote kheri tu.
Post a Comment