Leo Agosti 16 mwaka 2015 kulikuwa na mkutano wa madereva wa mabasi ulifanyika katika ukumbi wa Kimara
resort jijini Dar es salaam na kuahamua haya yafuatayo;
Kwa mujibu wa Naibu
katibu mkuu wa madereva (TADU), Rashidi Saleh aliwaeleza madereva hatima ya
kamati ambayo imeundwa na Waziri Mkuu kusuruhisha kero za Madereva hapa nchini.
Naibu katibu mkuu wa madereva (TADU), Rashidi Saleh akizungumza na madereva amesema "Tarehe
13 /8 tulipo kwenda baada ya wao kusikia kuna tishio la mgomo,tulizani kwamba
tunakwenda kujadili kwanini tunataka kugoma kwasababu tunazo kero zetu matokeo
tulikutana na ajenda ya mizani ya vigwaza ,tukakutana na matatizo ya wamiliki,
kamati kwenda Zambia kwenye ukaguzi wa mafuta, kamati kukagua spidi za magari
na timetable ya Sumatra wiki ijayo.Naibu Katibu TADU"
Pia alisema "Siku ya kesho Jumatatu Agosti 16 tutatoa tamko
kwa waandishi wa habari kuhusu hatima ya madereva wa Tanzania, vyombo vyote vya
habari kuanzia TV, Radio, Magazeti vitaonyesha kwahiyo kaeni karibu na vyombo vya
habari"
Amemalizia kwa kusema "Kuacha kuendesha
sio mgomo si umepumzika,Nani kasema mgomo sisi atugomagi uwa tunajipa
likizo vibarua uwa analikizo yake mwenyewe mpaka sasa sisi bado ni
vibarua. Sisi tunataka tuweke semina atakama ya siku tatu maana na sisi
tunahasira na ajali hivyo tutawaita walimu waje watufundishe na wale ambao wapo
Tunduma nao wasivuke kwasababu awatapata mafunzo maana redio haziskiki nje ya
nchi"
No comments:
Post a Comment