Advertisements

Friday, September 4, 2015

ATUPWA JELA KWA KUTOSAINI CHETI CHA NDOA CHA JINSIA MOJA

Image copyrightGettyImage captionKim Davies aliyekataa kusaini cheti cha ndoa Kentucky

Jaji mmoja nchini Marekani, ameagiza afisa mmoja wa serikali katika jimbo la Kentucky, kufungwa jela, baada ya kukataa kutekeleza agizo la mahakama la kutoa cheti rasmi cha ndoa, kwa wapenzi wawili wa jinsia moja.

Kim Davies amesema imani yake kama Mkristo, haimruhusu kusaini cheti kama hicho. Ndoa ya jinsia moja ilihalalishwa nchini Marekani Juni mwaka huu.

Umauzi huo wa Davis, wa kutosaini cheti hicho umepokelewa kwa hisia tofauti.

Kuna baadhi ya wale wanaomuona kama shujaa huku wengine wakisema ni msaliti.
Tofauti za imani

Davis ambaye ni karani wa mahakama, alikataa kutoa cheti hicho, kwa wanandoa hao katika kaunti ya Rowan iliyoko Kentucky.

Afisa huyo ambaye alichaguliwa na raia amesama, kitendo hicho kinakiuka maadili ya kidini.

Davis sasa ametupwa jela na jaji huyo kwa kudharau mahakama.


Amesema alikuwa amekula kiapo cha kuwa offisini na viapo vina maana nyingi.

Watu wanaoshabikia ndoa ya jinsia moja, walikusanyika nje ya mahakama, wakiimba kuwa mapenzi imeshinda na kusema kuwa sasa wanafuraha kwa sababu wanaweza kufunga ndoa.

Lakini kwa upande wake Kim Davis amepata uungwaji mkono kutoka kwa Wakristo wahafidina na baadhi ya wagombea wa urais wa chama cha Republican, ambao wanasema kuwa Davis amehukumiwa jela kwa kufuata imani zake.
bbc

7 comments:

Anonymous said...

Dunia imekwisha Jamani Duh..

Anonymous said...

Kwa mapenzi ya Mwenyenzi Mungu, usiogope wala usirudi nyuma Davis !

Mande P. said...

Huyo analifahamu neno la Mungu na alichofanya ni sahihi kabisaaaa!!!!!!! Ni kukosa vyote lakini Mbingu uipate,Mungu atampigania

Anonymous said...

Kama nimekufahamu vizuri yaani kutokana na wadhifa wake mama kwenye picha ya hapo juu amehukumuwa kwenda jela kwa kukataa kuidhinisha ndoa ya masenge au mashoga?

Anonymous said...

imekwisha kweli dunia na ole wao wala wasio wafuasi wa yesu;wasio mfuata aliyoyafundisha ya kweli na kuyafuata wanayoyataka wao ole wao.atakuja kuwakana wakae wakijua hilo.

Anonymous said...

Ati ndiyo nchi tunaambiwa ya demokrasia iliyobobea na inathamini na kulinda haki zote za binadamu!

Anonymous said...

It is a job. If she can't do it, quit!