ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 19, 2015

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kuwasilisha hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
 Mhe. Wilson Masilingi   Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho  Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.  Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi,  na Mkewe Marystella Masilingi.
 Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurejea nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kuwasilisha hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
Balozi Wilson Masilingi akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Marystella Masilingi na kushoto ni mtoto wao Nelson Masilingi

No comments: